Hatimaye Tessy Chocolate Afuta Tatoo ya Aslay.
Imekuwa ni kama kamchezo kanakojirudia kwa wasanii na watu wengi sana bila kujifunza kitu kutoka kwa wengine, mchezo huu umekuwa ukiwakumba watumbalimbali lakini kwa wasanii inaonekana sana kutokana na ukweli kwamba wao wanaonekana sana katika jamii.
Hivi karibuni kulizuka kwa maneno katika mitandao kwamba penzi la msanii aslay na mzazi mwenzake Tessy Chocolate limekufa na wawili hao hawapo tena katika mahsuinai na kwamba kwa sasa kila mtu ankaa kwao na kufguata utaratibu wake huku wakiwa na jukumu moja tu ka kulea mtoto wao.
Picha iliyotoka katika mitandao hivi karibuni ikimuonesha Tessy katika mkono wake ambao alichora tatoo yenye jina la aliekuwa mpenzi wake huyo Aslay kuwa imefutwa na katika eneo hilo kumechora ua, ukweli ndio unathibitika kuwa kumbe kweli wawili hao kwa sasa hawapo pamoja tena.
Wasanii wengi wamekuwa wakiathirika sana na uchorajiwa totoo za kudumu miilini mwao bila kujua kuwa mapezni muda wingine huweza kuwa na mwisho na ndipo wanapoanza kuangaika na kushora vitu vya ajabu kama maua na wadudu.