Jacqueline Wolper adai ataendelea kubadili wanaume kila kukicha

Muigizaji wa filamu za Bongo Jacqueline Wolper ako na tabia ya kubadili wapenzi kila kukicha. Na sasa amekiri kuwa hatawacha tabia yake hio.

Wolper alipokuwa na mahusiano na Harmonize watu wengi walidhani mapenzi yao yatadumu lakini wawili hao waliachana na kila mmoja kupata mpenzi mpya.

Wolper akiwa na mahusiano na Harmonize

Wolper alijinyakulia kichana mwingine mchanga anayejulikana kwa jina la Brown ilhali Harmonize alipata mpenzi mpya mrembo wa kizungu.

Katika mahojiano na Risasi Mchanganyiko hivi karibuni, Wolper alikiri kuwa ataendelea kubadili wapenzi muda wowote atakapogundua kuwa aliyenaye hana vigezo.

Wolper na mpenzi wake mpya Brown

Mrembo huyo alieleza kuwa hawezi kuogopa maneno ambayo watu wanasema kwani hawaelewi anachokumbana nacho katika mapenzi, alisema kuwa hawezi kung’ang’ania kukaa kwenye uhusiano ambao haendani nao au unampa shida.

“Unajua unapokuwa na mpenzi huwezi kujua kuna tabia utakumbana nazo ambazo haziendani na wewe, lakini pindi unapogundua ni bora kuondoka kuliko kukaa sehemu ambayo huna furaha nayo,” alisema Jacqueline Wolper.

 

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.