Johari Atokwa Povu Kuachana Kwa Ray na Chuchu hans

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Blandina Chagula maarufu kama Johari amejikuta akimwaga Povu Baada ya kuulizwa kuhusu kuvunjika kwa Penzi la Vicent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hansy.

Wiki iliyopita habari zilisambaa kuwa Msanii Ray na Mpenzi Wake wa siku nyingi ambaye pia ni mama wa Mtoto wake Jaden, Chuchu Hansy wameachana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  na Risasi Jumamosi, Johari alisema kwa mwaka huu hataki kabisa kuzungumzia maisha ya Ray na Chuchu kwa sababu yuko bize na mambo yake ya maisha na si kuangalia familia za watu wengine hivyo wanaosema amefurahia wawili hao kumwagana wamuache.

Yaani sitaki kabisa kuzungumzia masuala ya hao watu, kwa sasa nipo bize na mambo yangu na pia hayanihusu na wala siwezi kusema kwamba sijafurahishwa kwa kuwa sihitaji kabisa kujua na kufuatilia maisha yao”. Johari ameshawahi kuwa kwenye mahusiano ya miaka mingi na Ray ingawa walikataa kuwahi kuwa kwenye mahusiano hayo kwa muda mrefu.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.