Jokate Afurahishwa na Uteuzi wa Mh Rais.

Mwanadada mwanamitindo, mjasimiali, mwanasiasa na pia mkuu wa wilaya  wa Kisarawe ametoa yake ya moyoni baada ya mh Rais kufanya utezuzi wa viongozi wapya hivi karibuni huku akiwa na imani na uteuzi wa kijana Japhet Justice Sayi ambae bado kijana mdogo lakini kupewa nyadhifa kubwa serikalini.

Jokate amefunguka na kuona kuwa alichokifanya mh Rais ni jambo jema na kuwa amekuwa akionyesha vijana kuwa wanaweza kuleta mandeleo katika nchi na ndio maana ameazna kufanya kazi na vijana.

Katika ukurasa wake wa instagram, joate aliandika ”

Rais kaomba leo Ikulu uthibitishwe kijana mdogo uwe Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania. – TADB. 
“Tunaamini kwa akili na uwezo wako mkubwa sasa wakulima watafutwa machozi yao na hili la korosho utalisimamia vyema. Sina shaka na uwezo wako kabisa. Mwenyezi Mungu aendelee kukuongoza . 
“Asante Mhe Rais kwa kuendelea kuamini vijana wenye sifa na weledi kufanya vitu vikubwa kwa maendeleo ya nchi yetu,” ameandika Jokate kupitia ukurasa wake wa Instagram leo.
Japhet Justine Sayi alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyo kabla ya jana Rais Magufuli kuelelekeza Waziri husika anayeshughulikia benki hiyo kumthibitisha Rasmi kuwa Mkurugenzi mkuu

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.