Jokate Atangaza Ndoa Hivi Karibuni

Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006/07 na mfanyabiashara maarufu Jokate Mwegelo amefungukia nia yake ya kuolewa hivi karibuni.

Jokate ambaye ni mmiliki wa kampuni kubwa kabisa ya urembo inayoenda kwa jina la Kidoti, amefunguka hayo siku ya jana alipokuwa ansheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Ambapo kwenye ujumbe huo Jokate alifungukia harusi yake lakini pia aliongelea nia yake ya kuzaa watoto baada ya kuolewa.

Jokate alifunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika:

March Baby, March Queen soon to be somebody’s wife and mummy God is great and faithful, Grown but forever baby girl ni kwa Rehema na Neema tu”.

June mwaka jana katika mahojiano na Gazeti la Mtazania Jokate alisema anatamani umri ukifika apate watoto mapacha na wote awalee katika maisha ya kijijini na mjini ili wajue maisha ya pande zote mbili na kuweza kujifunza kilimo na kula chakula vya asili.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.