Kazi Yoyote Mpya ya Wema Sepetu kufungiwa.

Katibu Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo ,  Bi. Joyce Fisso amesema kama kuna kazi mpya ya Wema Sepetu inayotangazwa baada ya kufungiwa kujihusisha na kazi za filamu iripotiwe.

Fisoo ameiambia E- News  msanii huyo wamemfungia na bado wanaendelea kumfungia na wakitaka kumfungulia watafanya Press na waandishi wa habari kama walivyofanya awali.

“Wema tumemfungia na bado tunaendelea kumfungia, tutamfungulia kwa kutoa press kama tulivyofanya, kama nilivyosema tulisema tunafuatilia mwenendo wake na kweli tunafuatilia na kuna task ambapo tumempa tunazipima tukijiridhisha kuwa amerejea kwenye nidhamu na amejitambua tutakaa na kuona cha kufanya,” amesema Bi Joyce.

“Kama kuna kazi mpya mmeiona baada ya kufungiwa umeiona naomba iwasilishwe na utaona kitakachofuatwa.”

Maneno ya katibu huyu yanakuja baada ya kutolewa kwa uamuzi huo katika bodi hiyo kutokana na kosa la wema la kuvujisha picha za uchi.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.