CHAN 2025: Uko Ready Kujibamba Stadium?
Wasee, CHAN 2025 imekam mtaani!
Hii si yo match ya kawaida – ni vibe, ni sherehe, ni experience ya kufanywa lifetime memory.
Sasa kama unajua venye Kenya hushika moto kwa ball, hii ni chance yako ku represent – national colors na ku fly our flag high.
Hii ndio breakdown ya venye utabambika stadium bila stress – kutoka Kasarani hadi Nyayo.
Moi International Sports Centre, Kasarani
Hii ndio base fiti ya ball Nairobi. Kasarani ni kama national church ya ma fans.
Ukiingia hapa, utaskia ngoma kabla hata uone pitch.
Ngoma, vuvuzelas, flags, na moshpit za fans kutoka kila kona ya Kenya.
Hii ndio spot ya kufungua CHAN 2025, na pia final ya kufunga hii festival.
Uta enjoy aje hapa?
Fika mapema: Saa mbili kabla ya kickoff uko kwa gate. Unapata spot poa, na vibe huanza nje kabla game ianze.
Kaa na fans wa moto: Pale stand za kulia usually huwa na mabigi wa kuchant nonstop. Kama uko introvert, tafuta neutral zone 😂.
Tengeneza look: Cap ya Harambee Stars, face paint na custom bandana kwa kichwa.

Nyayo Stadium
Stadi ya roho safi. Hapa ni old school, pure passion.
Kama Kasarani ni king, Nyayo ni OG.
Iko karibu na CBD, so ni rahisi kufika. Na hapa ndio fans hujipanga kama familia – tight, loud, and proud.
Venye utacheza hapa:
After match: Tembea Upperhill au Railways Club for drinks na stories za ball. Ujipate tu kwa circle ya wasanii wakipiga story.
Viazi spot: Hapo nje kuna mama mmoja huuza viazi karai na achari ya ng’ombe. Ukikosa hiyo, utarudi for real.
Sakaja seats: Middle rows, unapata view safi na kelele inakufikia soft soft. Full experience.
Toka Game, Fika Experience
CHAN si game peke yake – ni culture, ni watu, ni sound.
Hii ndio time ya:
Kuvalia jersey – hata kama si team yako, show love.
Kujua chants – Wakilisha high school yako pale kwa cheering squad na chants, kama “Oyeee Kenya oyeee!”, lazima utambe nayo.
Kubeba squad – ball haina form bila maboys na magirls kucreate vibe.
Saa Ngapi Fiti Kuingia Stadium?
Game ikiwa 4PM, ingia stadium 2PM sharp.
Unaingia bila haraka, unapiga picha, unachukua spot ya hot, alafu una connect na atmosphere.
Na usisahau: watu huvaa red, green, black – patriotism ni lazima.
Na Usikose Hii Pia:
Fan zones : Kuna base za sherehe nje ya stadium with live DJ, giveaways, na influencers.
Graffiti & murals : pale Kasarani kuna art za Kenya, players, na fan quotes. Perfect for Insta.
Celebs : kutoka musicians, comedians hadi wanasiasa watakua hapo. Sijui kama utameet Nadia Mukami au Jalang’o kwa stand. Tujionee.
Ball Ni Sisi. CHAN Ni Yetu.
CHAN 2025 si ya kuwatch kwa TV pekee.
Ni ya kuishi, kufeel, kushout hadi sauti ipotee.
Tukionyesha Afrika venye Kenya hupeana stadium love, tunawacha legacy.
Jiandae bro, kam tujibambe.
Hii ni form ya nguvu ya kujienjoy na mbogi yako.
What you only need ni ticket, na ile energy ya mtaa.
CHAN ni sisi!
Tukutane stadium!