khadijanito Aliamsha Bifu na Mama Yake Mzazi

Mwaka 2017 msanii wa muziki wa bongo fleva Natasha Lisimo maarufu kama Khadijanito alifunguka katika kipindi cha Zamaradi Mketema kilichokuwa kikirushwa na Cloud Tv kuwa amekuwa katika bifu na mgogoro mzito na ndugu zake hasa mama mzazi kutokana na kitendo chake cha kubadilisha dini kutoka uislamu kwenda ukristo  akimfata mwanaume wake ambae amefunga nae ndoa.

Kipindi khadija akiongea hayo yote alikuwa ni majmizto wa miezi kadhaa, na alikuwa akiomba watu wasaidie kumuomba mama yake msamaha  ili aweze kumuelewa na kuelewa chaguo lake kuwa ndio maamuzi yake kubadili dini.

Baada ya msanii huyo kuumwa sana na kuzidiwa kipindi cha kujifungua mama yake mzazi alirudisha moyo wake nyuma na kumsamehe mwanae lakini tegemeo lake kubwa ilikuwa atakapopona mwane huyo atarudi kwenye dini yake na kuachana na mwanaume alimpeleka kwenye dini nyingine lakini kumbe hiyo ilikuwa tofauti kwa mwanandada kahadija ambae maamuzi yake hakutaka kuyabadilisha hata kidogo.

Inasemekana kuwa msanii huyo kwa sasa baada ya kujifungua bifu na mama yake mzazi limerudi palepale kwa sababu ya kurudi kule alipokuwa mwanzo ambako kulimfanya kugombana na familia yake.

Baada ya kutafuta ili kuthibitisha hilo khadija alikataa kuongelea swala hilo na kusema kuwa  ni mambo ya kifamilia zaidi.”vitu vingine sipendi kuviongelea sana  hususan maswala yangu na amam yangu ni maswala ya kifamilia zaidi .kama mnaniona ninajianika sana kwnye ukristo na ndio nilipoamua kuwa huko sidhani kama kuna haja sana ya kulizungumzia hilo.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.