Kisa Pesa, Christian Bella Ashindwa Kufanya Shoo.

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Christian Bella amefunguka na kukiri kuwa kwa sasa hali imekuwa mbaya na pesa hakuna na ndio ababu inayomfanya shindwe kufanya shoo mara tatu au nne kama hapo awali na kupunguza idadi ya shoo kwa mwezi na kufanya moja tu.

Bella anasema kuwa kwasasa atakuwa akifanya shoo mara moja kila jumamosi ya mwisho wa mwezi sio kama zamani na shoo hiyo itakuwa ikifanyika mzalendo pub iliyopo Kijitonyama.

mashabiki wangu najua kuwa mnapenda tufanye makamuzi kila siku na mara kwa mara lakini  kutokana na kwamba vyuma vimekaza sasa naomba tuwe tnafanya kila mwisho wa mwezi siku ya jumamosi  katika kiwanja hiki, :-Alisikika Bella alipokuwa akiongea na mashabiki wake alipokuwa katika shoo katika pub hiyo ya mzaleno iliyopo kijitonyama.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.