Kutambulishwa Sio Ndoa :-Mwijaku

Mahusiano kati ya Diamond Platnumz na Tanasha kila kukicha yanazidi kugonga vichwa vya habari, toka mwisho mwa mwaka jana yamekuwa yakichukua nafasi kubwa kwenye mazungumzo mtandaoni.
Kwa sasa ni mwigizaji wa filamu Bongo, Mwijaku ambaye amemueleza Tanasha kuwa asichukulie kitendo cha kutambulishwa kwa wazazi wa Diamond ndio tayari kaolewa kwani muimbaji huyo sio muoaji na ameshafanya hivyo mara kadhaa.
“Kutambulishwa sio ndoa, jiulize wangapi wametambulishwa kwa mama yake Diamond. Huu ni
utamaduni wetu wa Afrika ukitaka kuuteka moyo wa mwanamke mtambulishe kwa wazazi wako,” Mwijaku ameiambia Wasafi TV.
Mwishoni mwa wikiendi iliyopita Diamond na Tanasha waliibua  gunzo mara baada ya kusambaa kwa video mtandaoni ikionyesha Bibie akiwa na mama mzazi wa muimbaji huyo na dada yake, Esma Platnumz.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.