Kwanini Diamond ameshindwa kupost chochote kumtakia hali aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Zari

Mume wa Zari Hassan wa kitambo – Ivan Ssemwanga amelazwa hospitalini nchini Afrika Kusini. Ivan alikibizwa hospitalini baada ya kuugua ugonjwa wa Kiharusi (kwa Kiingereza stroke).

Siku chache zilizopita Zari aliwaomba mashabiki wake wamuombe mpenzi wake wa kitambo ambaye ni baba wa watoto wake watatu.

Soma pia: Zari awaomba mashabiki wake wamuombee mume wake wa kitambo – Ivan baada ya kulazwa hospitali kutokana na ugonjwa wa stroke

Zari alipoenda hospitalini kumwona Iva

Akiongea kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Diamond alieleza sababu zake za kukosa kupost chochote kumtakia hali Ivan Ssemwanga.

“Ni kweli mzazi wake Zari anaumwa, na yuko serious. Na kila siku huwa namuhimiza Zari akamuone mzazi mwenzie kwasababu najiuliza asingekuwa anaenda familia yangu ingemuonaje, kwa hiyo maskini dada wa watu kila siku huwa anaenda. Sijawahi mpigia simu kwasababu yuko serious sana na pia sikuweza kumpost kwasababu watu waneanza kusema labda natafuta kiki maskini ya Mungu kumbe wala,” Diamond alisema.

Diamond akiwa Clouds FM

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.