Lulu Amber na Jaguar kutoka Kenya kuachia wimbo pamoja?

Lulu Amber ambaye ni msanii mkubwa sasa kutoka Tanzania hivi karibuni alisema kuwa anamkataba na msanii kutoka nchini Kenya,Jaguar.

Amber Lulu

Muimbaji huyu alifunguka kudai kuwa Jaguar atakuwa anasimamia kazi zake wakati wowote anataka kuingia kwenye soko la Kenya.

Akizungumza na Showbiz xtra, ,Lulu alisema hili jambo la kujivunia kupata msanii kama jaguar kumpa shavu. Lulu aliendelea kusema kuwa hakuwa anatarajia jambo kama hilo kufanyika lakini anashukuru. Lulu alisema,

“Namshukuru Mungu kwa hili, nimepata mkataba mnono kwa Jaguar, makazi yangu yataendelea kuwa Bongo, lakini inapotokea nikahitajika Kenya nitakuwa nafika kwa wakati, niwaombe mashabiki wangu waendelee kunisapoti, naamini nitafika mbali zaidi na kuiwakilisha vyema nchi yangu,”

Hata hivyo bado anaendelea kufanya kazi zake za bongo.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.