Lulu Diva Adaiwa Kutupiwa Jini Baada Ya Kuiba Mume Wa Mtu

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘Homa’ Lulu Diva amedaiwa kutupiwa jini/ shetani baada ya kuiba mume wa mtu.

Habari hii inaripotiwa na Global Publishers ambapo inadaiwa kuwa ubuyu huo ulitolewa na mtu wa karibu wa Lulu Diva ambapo amedai kuwa alitupiwa jini hilo na mke wa mtu baada ya kumuiba mumewe miaka kadhaa iliyopita.

Chanzo hiko cha habari kimedai kuwa tangu ametupiwa jini hill amekuwa akipata mikosi mitupu na wanaume hiyo ikidhihirishwa na mahari yake aliyotolewa kurudishwa kwa mwanaume.

Baada ya tetesi hizo Ijumaa Wikienda ilimsakaa Lulu Diva na alifunguka mazito haya:

Kwanza naomba niseme huyo aliyewaambia nishamjua maana mimi mwenyewe nilimwambia alafu isitoshe mimi nilitoa siri hiyo kwa sababu kila mipango yangu ya ndoa ikikamilika kunatokea jambo na mwanaume anasema ana mambo yake mengine. Hapo kama sio kupigwa juju ni nini? Hilo la kwamba aliyenipiga juju ni mume wa mtu ni siri yangu”.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.