Lulu Diva Awatupia Dongo Zito Mavideo Queen

Mwanamuziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva anayefanya vizuri na kibao chake cha Ona, ameibua bifu zito na wauza nyago Kwenye video za wasanii (Video queen au video vixens).

Lulu Diva amewatupia Dongo Zito wale mavideo Queen wote ambao wanaacha kazi zao na kuamua kuongi Kwenye muziki wa Bongo fleva ambapo amedai sasa wameshapotea.

Lulu Diva alifunguka hayo Kwenye mahojiano na Global Publishers amesema kwamba, anaona kila dalili za wanadada ambao walikimbilia kwenye muziki wakitokea kwenye u-video queen wakipotea wote kwenye gemu jambo linalomfanya kujihisi kubaki bila mpinzani.

Wote wamepotea, siwezi kuwataja kwa majina nisije kuzua ya kuzua lakini sasa hivi hakuna video queen anayethubutu kubaki kwenye gemu zaidi yangu“.

Imekuwa kawaida kwa wasichana ambao wanafanya kazi kama mavideo Queen kujiingiza Kwenye Muziki ambapo wenyewe wamekuwa wakikiri kuwa mara ya kwanza walikuwa hawapati maslahi yoyote mfano wa mavideo Queen wanaofanya vizuri Kwenye Bongo fleva ni Gigy Money, Amber Lulu na wengineo kama Haitham.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.