Mafanikio Hayaambukizwi Kwa Njia Ya Kujaamina- Zari

Mwanamama mfanyabiashara maarufu Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ amewatolea povu zito wasichana ambao amedai ni wadangaji na kuwaambia mafanikio hayapatikani kwa njia ya kujaamiana.

Zari alitoa povu hilo siku chache zilizopita alipokuwa anamkumbuka Ex wake Ivan Semwanga aliyefariki dunia mwaka jana kutokana na maradhi ya ugonjwa wa moyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari aliandika ujumbe huo:

Pale unaposikia pesa za urithi…apo vipi Mafanikio hayaambukizwa kwa njia ya kujaamiana. .Endeleeni kudanga mkafikiri mwanaume tajiri atatokea man kukupa utajiri wa ghafla, na hata kama akiweza wewe utakuwa kama pambo ambalo anaweza akalitupa akinunua jipya lakini mimi sio rahisi kunitupa kwa maana mimi ni msingi na sio paa”.

Zari alitoa povu hilo baada ya kudaiwa pesa alizonazo ni za  Marehemu Ivan na sio Mali yake lakini Zari alianika picha zake za zamani na Ivan na kuwajulisha  watu wakati anaanza uhusiano na Ivan alikuwa hana hizo Mali hivyo walichuma wote.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.