Mboso Akanusha Kunyonywa na WCB.

Msanii kutokea WCB, Mbosso amesema hadi sasa fedha iliyotumika na lebo hiyo kwenye kazi zake haijarudi, hivyo hawezi kusema ananyonywa.

Muimbaji huyo kwenye mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema suala la kunyonywa kwake na WCB halipo kabisa. “Mimi leo hii nikisema nanyonywa , nitakataa kabisa kwa sababu nikijiangalia Mbosso wa mwaka jana hadi sasa najiona nimesogea hatua kubwa sana,” amesema.

Ukiachilia hilo mimi naona kama nawanyonya wao  kwa sababu hadi leo naweza kusema pengine pesa walizowekeza kwenye kazi zangu hata nusu yake sijairudisha bado,” amesema Mbosso.

Alipoulizwa ni ushauri gani anaukumbuka kutoka kwa Rich Mavoko, alijibu; “Kuna siku alishaniambia kuhusu kurekodi nyimbo tu, akaniambia ili uwe msanii mzuri hakikisha nyimbo zilizoko ndani ni nyingi kuliko zilizotoka,”

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.