Mchekeshaji Steve Nyerere awekwa motoni kutokana na sakata ya kimapenzi ya Wema Sepetu na Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Freeman Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai na Wema Sepetu wamekua wakitawala vichwa vya habari tangu sauti (voice note) ambazo zinadaiwa kuwa zao kuenea kwenye mitendao ya kijamii.

Voice note hio inaashiria kuwa Freeman na Wema Sepetu wana uhusiano wa kimapenzi lakini wawili hao walikana dhana hii.

Mchekeshaji Steve Nyerere amejipata pabaya kuhusu sakata ya Wema Sepetu na Freeman Mbowe. Mashabiki wa Wema na Freeman wanadai kuwa sauti ya kiume iliyoskika kwenye voice note hio ya utata ni ya Steve Nyerere.

Steve Nyerere na Wema Sepetu

Nyerere ako na kipaji cha kuigiza sauti mbalimbali za viongozi wa kisiasa na watu wengine mashuhuri; na  hii ndo sababu ya watu kumlimbikizia lawama.

“Sio mimi yule na siwezi kufanya kitu kama kile. Ile sauti ukiisikiliza kwa makini utajua sio mimi na siwezi kufanya hivyo,” Steve Nyerere alijitetea kwenye mahojiano na Bongo 5.

 

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.