Mfahamu Precious Aliyefanya Cover ya Diamond.
Mwanadada aliyejulikana kwa jina la precious amepata umaaarufu na kutrend katika mitandao baada yakuwa mwanadada wa kwanza kufanya cover ya wimbo wa diamond wa african beuty ulioimbwa na Diamond akimshirkisha omarion kuoka nje.
Sio rahisi kwa wasanii wengi wachanga Tanzania kuthubutu alichofanya dada huyu , huku wasanii wengi wakiona kama kugandamizia kazi za wasanii wakihisi kufanya hivyo ni kumpa kiki msanii husika.
Mwanadada huyu mwenye kipaji anahitaji kuangaliwa na wasanii wa wcb na kuona kama wanaweza kuendeleza kipaji chake kwa sababu amethubutu kufany wimbo mkubwa uliotamba kimataifa na hajaharibu hata kidogo.