Mimi ni Supa Staa Nitaishi Maisha Niliyoyachagua ila Nitaendelea Kuwa Humble kwa watu:-Alikiba

Msanii wa bongo fleva Alikiba anefanya vizuri na wimbo wake wa mvumo wa radi amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba yeye ni staa lakini amekuja akijali sana mashabiki zake kwa sababu ndio wanaomfanya yeye kuwa staa kila siku.

Alikiba nasema kuwa alichagua kuwa staa lakini hawezi kuishi maisha ya kuigiza kwa sabbau ya ustaa alionao na hii haitamfanya kuishi na watu vizuri kwa sababu eti yeye ni staa hata siku moja.

Alikiba ambae kila siku amekuwa akitaka kujishusha na amekuwa sio mtu wa kuongea kitu chochcote kuhusu mafanikio yake zaidi ya kuwashukuru mashabiki, anasema kuwa unapofanya kitu kizuri kitajitangaza chenyewe wala hakuna haja ya kutumia nguvu nyingi kutengeneza kiki ili ujulikana na jamii.

kuna maisha ya ustaa na kuna maisha ya kawaida kabisa, na kuna  maisha ya kuigiza kuwa staa,mimi ni staa na mimi ni supa staa na nitaishi maisha niliyoyachagua  lakini bado nitaendelea kuwa humble kwa watu.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.