Mkuu wa Wilaya Amezua Gumzo Baada Ya Kumpongeza Mumewe Kwa Kuoa Mke Mwingine

Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdallah amezua gumzo mtandaoni siku ya jana baada ya kumpongeza mume wake Abdallah Mohamed kwa kuoa mke wa pili.

Zainab amefunguka kupitia ukurasa wake Instagram na kumpongeza mume wake kwa kufunga ndoa na mwanamke mwingine ambaye anakuwa mke mdogo.

Asalaam Aleykum, Nichukue nafasi hii kumpongeza mume wangu kwa kuongeza mke wa pili. Kwa kuwa dini yetu ya kiislamu inaruhusu, wazo la kufanya hivyo lilitoka kwangu kulingana na uzito wa majukumu yangu nalazimika muda mwingi kuwa mbali na nyumbani na hivyo mume wangu kukosa huduma za msingi. Namshukuru kwa kunielewa na kulifanyia kazi ombi langu hatimaye nimepata mwenzangu wa kusaidiana nae majukumu mazito ya ulezi wa mume”.

Lakini pia aliendelea kuandika:

Alhamdulilah, M/Mungu ametupa riziki na uwezo hivyo tunapaswa kutumia rehema hizi na wengine, mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe , yaarab atupe stara inshallah karibu kwenye familia mke mwenzangu karibu Kwenye familia na nimekupokea kwa mikono miwili na Mwenyezi Mungu atupe masikilizano na tuishi na mume wetu kwa wema mpaka Jannah”.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.