Monalisa Afungukia Bifu La Wema na Riyama

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Monalisa amefunguka na kuongelea bifu lililosemekana lili kuwepo kati ya waigizaji wawili wa Bongo movie ambao ni Wema Sepetu na Riyama Ally.

Wiki chache zilizopita Wema alichukua tuzo ya Muigizaji bora wa kike kwenye Bongo movie Kupitia Tuzo za SZIFF ambayo alishindanishwa na wasanii wengi kama Riyama.

Baada ya Riyama kukosa tuzo ile alifanya Interview na kituo kimoja cha redio na alimwaga machozi live  kabisa huku akidai kuwa yeye alistahili kupata tuzo ile na kuwataka SZIFF wamuombe radhi kwani kukosa kwake tuzo ni Kumdhalilisha.

Baada ya kuongea maneno hayo moja kwa moja ilivhukuliwa kuwa Riyama amejijengea bifu na Wema Sepetu kwani ni sawa na alisema kuwa Wema hakustahili kupata tuzo hiyo.

Lakini Riyama na Wema walizima tetesi hizo za kuwa na bifu baada ya kupiga picha pamoja wakiwa Airport walipoenda kumpokea Monalisa ambaye alikuwa ametoka kuchukua tuzo yake nchini Ghana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm Monalisa alifunguka haya kuhusiana na maneno yaliyosemwa kati ya Wena na Riyama:

Kwanza niseme nilivyofika pale sikutegemea kuona watu lakini nilivyoshuka nikakutana na wasanii wenzangu, nilijisikia furaha sana..

Nilifurahi kuawaona, sidhani kama Riyama kamlalamikia Wema nyie tu ndio mnachukulia vibaya, Riyama alikuwa na malalamiko yake na mimi ninayafahamu toka siku ya kwanza”.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.