“Mungu Atanipa Mume Wa Kunioa”- Hamisa Mobetto

Msanii wa Bongo movie na mfanyabiashara Hamisa Mobetto ameibuka na kudai Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayeweza kumpangia mume wa kumuoa.

Hamisa ambaye amezaa mtoto mmoja na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amedai mwanaume ambaye atakuja kuwa mume wake wa ndoa anapangiwa na Mwenyezi Mungu na sio mashabiki wa mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano na gazeti la Ijumaa Wikienda, Hamisa amesema yeye ni mwanamke na kamwe hawezi kupinga kuwa atakuja kuwa mke wa mtu, lakini yote hayo yanapangwa na Mwenyezi Mungu na siyo dua za binadamu.

Watu wanashindwa kuelewa kwamba hakuna kitu sisi wanadamu tunajipangia bali muumba wetu, kwa hiyo hata mimi mume wangu atakayenioa anapangwa na yeye maana wenye kutabiri ni wengi na siyo kwamba ukizaa na mtu ndiyo lazima akuoe yeye”.

Hamisa ambaye kwa sasa ameachana na aliyekuwa mpenzi wake na Baba watoto wake Diamond Platnumz ameonekana Kupitia changamoto nyingi sana za kimapenzi.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.