Mwanakheri na Niva Ndani ya Bifu Zito.

Wasanii wa bongo movies Niva pamoja na Mwanakheri wanasemekana wapo kwenye bifu zito ambalo limesababishwa na msanii mwenzao Riyama Ally.Baada ya kuchunguza kwa muda mrefu ilikuja kubainika kuwa wasanii hao wawili wapo katika bifu zito kwa  zaidi ya miaka miwili.

Sababu kubwa ya wawili  hao kuwa na bifu ni baada ya niva kumkataza mwanakheri kuwa anamtukana Riyama Ally kwa sababu yeye ndio aliemtambulisha katika tasnia ya maigizo.

Kampuni ya GPL  waliamua kumtafuta Niva ili aweze kuthibitisha swala hilo ambapo alikiri kuwa ni kweli yeye na Mwanakheri hawapo katika mahusiano mazuri na hii yote ilitokana na yeye kumkanya msanii huyo kuacha kumtukana mwenzake kwa kuwa ndie aliemtambulisha katika game.

Hata hivyo baada ya kumtafuta mwanakheri kumuuliza swala hilo alikana na kusema kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu yeye kumtukana Riyama na hata huyo Niva hawaingei kwa sababu sio rafiki yake.

Sijawahi kumtukana riyamma,na huyo niva hajawahi kunirekebisha kwa kitu chochote  ila sipo nae kribu kwa sababu sio rafiki yangu.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.