Mwendesha mashtaka akaribia kukamilisha uchunguzi wa kesi ya Wema Sepetu kuhusu biashara ya mihadarati

Upelelezi wa kesi ya Wema Sepetu kupatikana na bangi unakaribia kukamilika. Msanii huyu maarufu wa filamu za Bongo alikamatwa na polisi mapema Februari baada ya kupatikana na misokoto ya bangi nyumbani kwake.

Wema Sepetu aliachiliwa kwa dhamana Februari 6 baada ya kuzuiliwa jela kwa muda wa siku sita. Kesi yake ilitajwa mahakamani lakini mwendesha mashtaka aliomba mahakama impe muda kukamilisha upelelezi.

Wakili wa serikali Constantine Kakula alieleza mahakama (Jumatano) kwamba upande wa mashtaka ulikua katika hatua za mwisho kukamilika upelelezi wao.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, hakimu wa mahakama ya Kisutu aliuhimiza upande wa mashtaka wajitahidi kuukamilisha upelelezi, kesi hio imeahirishwa hadi Aprili 11, 2017.

Wema Sepetu na meneja wake Martin Kandinda wakitoka mahakamani

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.