Nakaaya Sumari Afungukia Sababu Za Kuacha Muziki

Nakaaya Sumari alijizolea umaarufu miaka michache ya nyuma baada ya kuachia wimbo wake uliofanya vizuri ‘Mr. Politician’ Lakini pia alijulikana Kupitia mdogo wake Nancy Sumari aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2005.

Kwa miaka mingi Nakaaya amekuwa kimya na Kupitia kabisa Kwenye muziki lakini Jambo ambalo watu wengi hawalifahamu ni kwamba kilichompoteza ilikuwa ni ajali mbaya aliyoipata mwaka 2011, kiasi kwamba mgongo wake ukaharibika vibaya na kumaliza miezi mingi akiwa amelala kitandani bila kufanya lolote lile.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Nakaaya ameweka wazi kuwa ameacha muziki na kufunguka zaidi yafuatayo:

Kiukweli kwa sasa nimeacha muziki kwa sasa nina mambo mengi ya kufanya. Nina kampuni yangu ambayo inahusika na mambo mengi ikiwemo chakula, ndiyo nadili nayo kwa sasa”.

Lakini pia Nakaaya aliulizwa kuhusu wasanii wa Bongo fleva na yupi anayenvutia kwa sasa;

Ninasapoti wanamuziki wote. Kiukweli wanafanya vizuri na muziki unakua na unakwenda mbali“.

 

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.