“Nakupenda Sana, Kula Ushibe Halafu Kaza Chaga”-Dogo Janja

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja ameibuka na kumtumia ujumbe Mpenzi wake  Mpya anayejulikana kwa jina la Linah.

Dogo Janja alitangaza kuchana na aliyekuwa mke Wake Msanii Irene Uwoya mapema mwaka jana Baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miezi kadhaa.

Dogo Janja Hivi sasa yupo kwenye mahusiano na Mrembo ambaye ni Mfanyabiashara kutoka Arusha ambaye anasemekana kuwa na pesa ndefu kutokana na Familia yake kuwa kwenye biashara za madini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dogo Janja amemtumia ujumbe wa birthday mrembo huyo ambaye alizaliwa siku ya jana:

Hakuna neno linaloweza kutosha kuielezea furaha niliyonayo kwenye kufurahia siku yako ya kuzaliwa mpenzi wangu…..mengine nitakueleza chumbani…..kula ushibe kisha kaza chaga….nakupenda sana”.

https://www.instagram.com/p/BtlyFosFIt9/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1tdljljimtqu5

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.