Nandy Adai Yeye Ndio Msanii Mkali Wa Kike Bongo

Staa wa muziki wa Bongo fleva anayeendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Ninogeshe’ Faustina Charles ‘Nandy’ ameibuka na kusema yeye ndio Msanii was kike anayeongoza Bongo.

Nandy amefunguka na kudai anaamini kuwa kwa sasa yeye ndio msanii wa kike ambaye amekuwa consistant na kushika chati za juice kutokana na ngoma anazotoa.

Kwenye Interview aliyofanya na Clouds Tv, Nandy amekiri kuwa yeye ni namba kwa kigezo cha namba ila anawaheshimu wale wote waliomtangulia kimuziki.

“Namba moja kwa Tanzania sasa hivi, au wewe unaonaje?, go with numbers, go YouTube, go Subscriber, go every where, go with numbers. Usiangalie tu nani anafanya nini, angalia numbers.

Kabla sijawa namba moja, namba moja yangu Lady Jaydee lakini bado nitamuheshimu, ni mkubwa amenitangulia. Yeyote yule ambaye amenitangulia lazima nimuheshimu kwamba ni mkubwa”.

Lakini pia Nandy amesema ingawa kuna wasanii wengi wakongwe anaowaheshimu kama Lady Jay Dee lakini haimaanishi wao watakaa Kwenye chati milele lazima wapishane kila mtu kwa nafasi yake atabeba chati.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.