Nelly Kamwelu Yupo Njiani Kufunga Ndoa

Mlimbwenda ambaye amewahi kushikilia mataji mbali mbali ya urembo hapa nchini ikiwemo Miss Universe Tanzania, Nelly Kamwelu amesema yupo njiani kuolewa.

Nelly amefunguka na kuweka wazi kuwa mwanaume anayetarajia kumuoa hivi karibuni sio mtu maarufu lakini ni mwanaume ambaye amekuwa naye kwenye mahusiano kwa muda mrefu sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Nelly alisema kuwa anamshukuru Mungu ameweza kumpata mtu ambaye anam­penda na anaahidi kuwa mke bora baada ya tukio hilo la heri kukamilika.

Unajua kila jambo na wakati wake, yamesemwa mengi juu yangu lakini nashukuru Mungu siku si nyingi nitaandi­ka historia katika mai­sha yangu, kwa lugha nyingine ni kwamba naolewa ‘soon’ kwani nimeshachumbiwa”.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.