Nimekoma Kuwa Kiongozi Msibani.;- Steve Nyerere

Msanii maaru­fu wa vichekesho Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema amekoma kuwa kiongozi misibani kwa sababu ya matusi anayovuna akishika nafasi hiyo.

Steve aliiambia Za Motomoto News wikiendi iliyopita kuwa, amekuwa akijitoa kwenye misiba ya wasanii wenzake lakini licha ya wema wake huo amekuwa akivuna skendo za ajabuajabu (kama ulaji fedha za rambirambi) na matusi jambo ambalo linamhuzunisha na kuiathiri familia yake.

Unajua mimi nina wa­toto, sasa wanapoona ya­nayoandikwa mitandaoni ya kunitukana na kunifedhehesha kwa vitu vya uongo wa­tanichukuliaje, niseme tu huu msiba wa mtoto Patrick Peter ambaye ni mtoto wa msanii mwenzangu Muna ndiyo wa mwisho, sitajihusisha tena na uongozi; kwenye misiba nita­shiriki kama mtu wa kawaida,” alisema Steve.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.