Nisha Kulia Na Wanaoiba Mabwana Za Watu

Nisha amekuwa ni moja wa wasanii wa kike ambao kila siku wanalalamika kutokana na wanawake wenzake kumtesa kwa kumuibia wanaume anaokuwa nao kwenye mahusiano.Sio mara ya kwanza  Nisha amekuwa akilalamika kuwa kuna nyakunyaku mjini wamekuwa wakiharibu usingizi wake kila kukicha kwa kumuibia wanaume.

Hivi karibuni alikuwa katika mahusiano na mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la ,inu ambapo baada ya kukaa katika mahusiano kwa muda, zilizuka tetesi kuwa mwanaume huyo na Nisha wameachana ambapo baada ya Nisha kutafutwa na vyombo vya habari alikana na kusema kuwa hizo tetesi ni za uongo na kwamba hawajaachana na mpenzi wake huyo.

Lakini kama kawaida mitandao ya kijamii huwa haina siri, hivi juzi Nisha alishindwa kuvumila hilo na kuanza kuposti baadhi ya captions zilikonyesha kuwa tayari alishaumizwa na mwandani wake kutokana na kulalamika kwa kutesa na mapenzi.

Nisha ambae alilalamika katika ukurasa wake wa insta na kusema kuwa kila siku yeye amekuwa ni mtu wa kuibiwa mabwana na kwamba ameshachoka na kitendo hicho na kumalizia kuwa kwa sasa hana haja ya kumuanika mpenzi wake katika mitandao ili aweze kuficha watu wasimjue wasijewakamuiba tena kama alivyoibiwa yule aliyepita.

Lakini moja ya vitu vya kuajabisha ni kwamba mwanaume aliyekuwa nae katika mahusiano , Minu alijibu kwa kusemakuwa ‘”Mwanamke akimwga mbona wewe usimwage ugali, chukua dekio ufute“‘

Hata hivyo Nisha alipotafutwa na gazeti moja kuhusu vijembe hivyo na malalamiko yake  aliishia kucheka na kusema kuwa ‘”jamani kwani hapo ndo nimesemakuwa nimepata mwingine, hahaha‘”

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.