Penzi la Harmonize na Sarah Linapumulia Mashine

Penzi la staa wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize na mpenzi wake mzungu Sarah limedaiwa kuwa linapumulia mashine baada ya kugombana wikiendi iliyoisha.

Kupitia mitandao ya kijamii Harmonize na Sarah walidhihirisha kuwa katika mafarakano baada ya Sarah kumwaga povu Kwenye ukurasa wa Instagram wa Harmonize.

Huku sababu juu ya kugombana Ikiwa ni wivu wa kimapenzi, Sarah alionekana kuona wivu baada ya Harmonize kuposti picha akiwa na mwanadada ambaye ni mtangazaji nchini Nigeria anayejulikana kama Nancy Isime, ambako Harmonize ameenda kikazi.

Basi Sarah akiwa nyumbani wivu ukamshika alipoona picha hiyo alianza kumshushia matusi ya nguoni Harmonize huku akimjulisha yule mdada  kuwa yeye ndiye mwanamke halali wa Harmonize.

Baada ya povu hilo kuendelea basi Sarah akahamia kwa mwanadada aliyekuwa na Harmonize akampa na yeye vya kwake kuonyesha kukabwa na wivu uliopitiliza.

Baada ya sakata hilo Harmonize alitangaza yeye na Sarah wameachana baada ya kuposti kwenye ukurasa wake wa Snapchat kuwa yupo single:

 

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.