Petit Man Afungukia Tetesi Za Kufulia Mpaka Kuweka Bondi Passport

Mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva Petit Man Wakuache amefunguka na kukana tetesi zinaendelea kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefulia.

Petit Man ambaye ni mume wa Esma Platnumz dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amekana taarifa za yeye kufulia mpaka kuweka passport yake ya kusafiria rehani.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Petit amesema taarifa hizo ni za uongo na zinasambazwa na mtu ambaye ni mbaya wake ambaye anapenda tu kumchafua;

Sijawahi kufanya kitu hicho ndio maana hata sikuwahi kukizungumzia kwa sababu hates wako wengi sana, kuna watu wengi wanachuki na maisha yangu lakini sio habari za kweli na sijawahi hata kuitwa na Migration kwaajili ya hiyo ishu”.

Tetesi za Petit Man kufulia zilipamba moto hasa pale alipodaiwa kuweka ndani polisi baada ya kushindwa kulipa deni shilingi milioni 10.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.