“Prezzo Anampenda Amber Lakini Tatizo Hajatulia”- Gigy Money

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefungukia penzi la shoga yake Amber Lulu na mpenzi wake Prezzo.

Siku za hali karibuni kumetokea sintofahamu Kwenye penzi la Msanii Amber Lulu na mpenzi wake Msanii kutoka Kenya Prezzo ambapo imesemekana wawili hao wameachana.

Lakini utata zaidi ulitokea siku mbili hizi baada ya picha kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Prezzo akiwa na mwanamke mwingine wakiwa kitandani.

Baada ya skendo hiyo Amber alitumia mitandao ya kijamii kutangaza kuwa amelitua Penzi lake na Prezzo na kuweka wazi kuwa kwa hivi sasa yupo single.

Kwenye mahojiano na XXL ya Clouds Fm, Rafiki wa karibu wa Amber, Gigy Money amefunguka na kudai Prezzo anampenda Amber Lulu Lakini tatizo lake hawezi kuacha michepuko:

Yaani mshakji (Prezzo) anampenda Amber Lakini ndio hivyo ana mambo mengi yaani amefanya vitu vya ajabu sana rafiki yangu kwa rafiki yangu yaani ana mademu kibao na hivi wapo mbali basi ndio vituko kibao”.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.