Q-Boy Msafi Afunguka Baada Ya Fumanizi Lake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Q-Boy Msafi amefunguka baada ya kufumaniwa na mpenzi wake Wikiendi iliyopita ambapo amedai kuwa anaona aibu sana baada ya sakata hilo.

Siku chache zilizopita kuna video ilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Q- Boy akiwa anatembezewa kichapo  na mwanamke mmoja aliyetajwa kuwa ni mpenzi wake.

Video hiyo ilichukuliwa wakati Q- Boy akiwa saluni na mwanamke mwingine ambaye inasemekana kuwa ni mchepuko wake lakini mambo yaliharibika baada ya mpenzi wake kuingia na kuwakuta ndipo alipoanza kukunjwa na kutembezewa makofi na mpenzi wake.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Enews cha EATV, Q-Boy amedai amesikitishwa sana na ile video lakini  mwanamke yule sio shuga mama wake kama taarifa zilivyoenea kwenye mitandao ya kijamii:

Yule ni mwanamke ni mshkaji wangu ambaye tunasaidiana kimawazo tu katika life Lakini sio kwamba ananipa pesa au anafanya huduma zozote kwangu mimi mtoto wa kiume napambana mwenyewe”.

Lakini pia Q-Boy amesisitiza kuwa hana uhusiano wowote na wanawake wale:

Kwenye mitandao zinasambaa habari nyingi sana ambazo sizo za ukweli na ukweli ni kwamba wale ni washkaji zangu na kilichotokea pale ilikuwa ni misunderstandings tuu sio kiki na kilichotokea naona aibu sana na naomba mashabiki zangu wanaielewe mimi sio mtu wa kugonganisha wanawake”.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.