Q-Chillah Arudi Mzigoni, ni Baada ya Kutoa Ngoma Mpya
Baaada ya kutangaza kuacha muziki na kupatawadau wengi sana waliomlilia na kumuomba sana kuacha habari za kutaka kuacha muziki msanii Q- Chillah aliamua kufuata ushauri wa mashabiki na wadau wakubwa wa muziki na kuendelea na kazi hiyo.
Hivyo msanii huyo kwa kipindi cha muda mfupi huo maeweza kutoa wimbo mpya jana kwa kuuachia katika vituo vy habari na burudani ngoma yake hiyo inayokwenda kwa jina la kisamvu.
Sio rahisi kwa mtu aliyekata tamaa kurudi tena katika muziki kwa kishindo kikubwa lakini bado mashabiki wa msanii huyu bado wana imani na kipaji chake kikubwa hivyo wanaamua kuendelea kumsapoti.
Video hiyo iliyotengenezwa na kwetu studio itakuwa na usimamaizi wa Alpha Chain international.