Queen Darlen Amkana Alikiba Kweupe

Mwanadada Queen Darlen ameamua kufunguka na kusema kuwa hana ukaribu wowote na Alikiba zaidiya kwamba walikuwa wakifanya kazi pamoja na hiyo yote ilikuwa ni kwa sababu walikuwa chini ya uongozi unaofanana.Queen Darleen amesema huwa anapoulizwa na media kuhusu Alikiba hapendi kumzungumzia kwa madai kuna watu watatafsiri tofauti.

Wasanii hao ambao mwanzoni watu walidhani ni ndugu walishafanya wimbo pamoja na Queen Darleen amesema ni kwasababu kipindi hicho yeye na Alikiba wote walikuwa chini ya label moja. Queen Darleen amesema Hana ukaribu wowote na Alikiba tangu zamani ilikuwa ni kazi tu

Pia akizungumza na GPL Queen Darleen amesema wakati anaanza muziki takribani miaka 15 iliyopita hakupata usumbufu wa rushwa ya ngono toka kwa wanaume walio kwenye tasnia Kama baadhi ya wasanii wa kike kwasababu yeye alishikwa mkono na Dully Skyse kwa hiyo akizinguliwa tu kwa mambo ya kijinga alikuwa akimwambia Dully .

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.