Ray c Amganda Kooni Hamisa Mobeto.
Mwanadada Ray c amezidi kuonyesha kumchukia msanii mwenzake Hamisa Mobeto kutokana na kuwa anamponda na kumkebehi hasa baada ya Hamisa Mobeto kutoa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la madam hero ambao umeanza kusikia sehemu mbalimbali.
Katika ukurasa wake wa instagram, Ray c aliandika cooment ambayo likuwa haina jina la aliyemlenga lakini inavyoonekana ni kama alimlenga Hamisa kwa sababu ni siku hiyo ndio wimbo ulikuwa umeanza kusambaa lakini pia kutokana na historia kuwa mwanadada huyo amekuwa akirusha mabomu kwa mwanadada mwenzake.
Ray c aliandika “MNAHARIBU MAANA NZIMA YA BONGO FLAVA, ACHENI UTANI NA KAZI ZA WATU, SIO LAZIMA KILA MTU AIMBE ITS A BULLSHITS’
Mara nyingine nyingi Ray c amekuwa akiweka posts ambazo zinahashilia kumponda hamisa , mfano aliwahi kumponda kwa kumkebehi sana kuhusu duka lake la nguo na fashion analomiliki Hamisa.