Roma Atasitisha Zoezi la Kutoa Nyimbo Baada Ya Brazil Kufunga

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Roma Mkatoliki amesema anafuata ahadi yake na kusema hataweza kutoa nyimbo kwa sababu Brazil wameshinda.

Siku ya leo kabla ya mechi ya Kombe la dunia kati ya Mexico na Brazil  Roma alitangaza Kupitia Kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa endapo Brazili akifungwa basi ataachia ngoma yake mpya.

Na baada ya matokeo kutoka na Brazil kumfunga Mexico Roma aliweka wImazi kuwa hataweza tena kuachia wimbo mpya.

Lakini Kama Utakumbuka katika michuano ya mwaka 2014 Roma aliahidi endapo Brazil itafungwa na Ujerumani atahama Tongwe Records na kwenda Sharobaro Records.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.