S2Kizzy Anena na Wanaosimamaia Sanaa.
Mtayarishaji wa nyimbo mablimbali nchini kutoka Switch Record amefunguka na kulalamikia mamlaka zinazosimamia sanaa kwa kile kinachodaiwa kuwa wamekuwa wakiwasahau sana ma-producer katika kila jambo wanalopanga kuhusu sanaa.
S2kizzy anasema kuwa ni vigumu sana kwa watayarishaji wakubwa nchini kuwa na maisha mazuri kama nyimbo zinazotengenezwa na kuwa kubwa hata haifikii kiwango cha maisha wanayoishi wao.
ni vigumu sana wasanii wa nje kufanya kazi na ma-producer wa nchini, lakini utaona inavyoendelea kusikia kuwa wasanii wa ndani wakitoka kufanya ngoma nje,na hii yot ni kutokana na mazingira yalivyoweka na mamlaka husika.
S2kizzy anasema kuwa moja kati ya ma-producer bora kwake ni mt t touchez ambae amekuwa akifanya vizuri sana kwa kipindi chote hata kufikia hatua ya kusaidia sana vijana wengine wegi katika game la muziki.