Shetta Adai Mtoto Wake Amezaliwa Staa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nurdin Bila maarufu kama Shetta ameibuka na kudai Mtoto Wake Qayla ana ustaa wa kipekee ni tofauti na watoto wa mastaa wengine ambao wametengenezwa kuwa mastaa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Shetta amesema umaarufu ambao mtoto wake anao mpaka sasa hajahusika hata kidogo kuutengeneza kwa maana hajawahi kutumia muda wake mwingi kumtangaza wala kumfanyia mtoto wake kitu chochote ambacho kingefanya jamii imfahamu au kufatilia kile anachokifanya.

Kwa kweli umaarufu wa mwanangu Qayllah hata mimi mwenyewe unanishangaza kwa maana kila siku zinavyozidi kwenda nashangaa anafanya vitu ambavyo vinafanya watu wazidi kumpenda, yaani mpaka sasa naona kama anataka kuzidi jina la Shetta sasa maana watu wananiita baba Qayllah badala ya jina langu”.

Hivi sasa Shetta na mke Wake Leila  wana watoto wawili ambao wote ni wa kike ambao ni Qayla na Qamrah.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.