Sister Fey Atetea Penzi Lake na Kibenten Awashukia Wanaotaka Kumnyakulia

Msanii wa Bongo fleva Faidha Omary maarufu kama Sista Fey ameibuka na kutetea Penzi lake na kibenten chake Msanii anayejulikana kama Hollystar.

Sista Fey amewajia juu watu ambao wamekuwa wakikosoa Penzi lao kisa Umri na hata kumtuhumu kwa kumbemenda kijana huyo ambapo Fey amedai umri ni namba tu na hakuna kingine na zaidi yeye anaona wameendana.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda , Sister Fay’ alisema kuwa, katika ulimwengu wa sasa suala la umri ni namba na halina tatizo kwenye uhusiano na kwamba amewashitukia wote wanaomsemasema kuwa kunakitu wanakitaka kwa mpenzi wake huyo.

Wanaonisema mara sijui ninambemenda mpenzi wangu wanataka kunipora na hakuna lolote, kwani simbemendi na mimi nina uhakika tunaendana”.

Sista Fey na mpenzi wake Hollystar wamejizolea umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii kutokana na vituko vyao wanvyofanya.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.