Skyner Awachana Mastaa Wanaopenda Kukopa

Msanii mkongwe wa Bongo movie Skyner Ally ameibuka na kuwachana mastaa ushuzi ambao wamekuwa na tabia ya kwenda kukopa bidhaa Dukani bila kulipa.

Skyner ambaye ni mmiliki wa boutique nguo na bidhaa mbali mbali lililopo Kinondoni studio amewatolea povu mastaa ambao wamekuwa na tabia ya kukopa bila kulipa.

Skyner amewamwagia povu zito na kuwaonya kuwa endapo hawataenda kumlipa basi atakuwa hana jinsi bali ni kuwanika hadharani maana kuna wengine hawapatikani kwa simu huku wengine wakiwa wamemblock:

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani, Skyner amesema anaumia kwa sababu anatafuta kwa taabu sana lakini anashangazwa na baadhi ya watu ambao wengine ni mastaa wanamkopa lakini mwisho wa siku wanamzungusha.

Inaumiza, mtu unahangaika na jua huku na kule halafu mwingine anakuja kukukopa halafu anaingia mitini aisee inauma sana, nikiona inazidi kwa kweli nitawachana live kabisa maana wengine wana majina makubwa lakini wanajitia kichwa ngumu”.

 

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.