Snura Awakingia Kifua Singo Mamaz

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchi, Snura Mushi ameibuka na kuwasifia wanawake wote ambao wamekuwa wakilea watoto wao  bila kumtegemea mwanaume katika maisha yao.snura anasma kuwa mwanamke wa dizaini hiyo  anakuwa amepata elimu tosha ya Dunia kutokana na magumu anayoyapitia kwa sababu maisha ya kuwa singo mama ni magumu sana.

Snura anasema kuwa yeye ni mmoja kati ya kina mama walioweza kuwalea watoto wakiwa peke yao na amepitia changamoto nyingi sana mpaka sasa watoto wake wamefika umri mzuri lakini pia amejifunza mengi sana katika kulea watoto hao na amejikuta anakuwa jasiri sana na anaweza kusimama popote .

Yaani kulea watoto mwenyewe kama mwanamke ni jambo la ujasiri sana, na ni elimu tosha kabisa, mimi najivunia hilo kwa kweli.mwanzoni ilikuwa ngumu sana kwa sababu sisi wanawake tumekuwa tukiwategema wanaume mara nyingi wakiwepo lakini ukiyajaribu maisha ya ulezi ukiwa peke yako na ukaweza kuashinda basi ujue unaweza kuingia popote.

Hivyo Snura anawapa hongera wanawake wote ambao wamekuwa mstari wa mbele kuwalea watoto wao bila kuwa na utegemezi wala kulia lia shida juu ya maisha kuwa magumu kutokana na kulea watoto wao.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.