Tabasamu la Feza Kessy Lilivyompatia Mpenzi Alienae.

Msanii wa Bongo Fleva Feza Kessy amefunguka kuwa wanaume wengi anaoingia nao kwenye mahusiano wanapenda cheko lake.

Feza amefafanua kuwa hata yeye alikuwa hajui kama anacheka vizuri kiasi cha kufanya wanaume kupagawa juu ya cheko hilo

Akizungumza na EATV Feza amesema, amegundua hilo baada ya kukutana na maoni mengi kuhusu cheko lake, pia wanaume wengi anaokutana nao kitu cha kwanza kukisifia juu yake ni kicheko. “Mwanzo nilikuwa najua watu wananitania tu, ila bwana kila mwanaume nayempata unakuta anapenda cheko langu lakini mwanzo ilikuwa ngumu kuamini kuwa wanaume wengi wanapenda kicheko changu, lakini kwa sasa hivi naamini hata mpenzi wangu ndio kitu kikubwa anapenda”,amesema Feza kessy.

Lakini Feza ameingiwa na hofu kwa kusema kuwa muda mwingine hafurahii kuona wanaume wengi wanampendea hicho kitu na anaogopa siku akiwa hana hicho kicheko itakuwa rahisi kuachika.

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.