Tanzia- Msanii Sam Wa Ukweli Afariki Dunia

Msanii wa Bongo fleva Sam wa Ukweli aliyefanya vizuri na vinaigrette vyake kama ‘Kwetu wapo’ na sina raha amefariki dunia.

Sam wa Ukweli ameaga Dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Palestina Sinza baada ya kuugua kwa muda mrefu, mwili wa marehemu umepelekwa katika hospitali ya Mwananyamala.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv, Producer wa marehemu Steve aliyekuwa akifanya kazi na Msanii huyo alifunguka kuhusu maradhi yaliyokuwa yanamuandama marehemu:

Sam alianza kuzidiwa tokea J’mosi, tulipomuuliza anaumwa nini alisema UKIMWI lakini sio Ukimwi wa kawaida bali ni ukimwi wa kulogwa”.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina. R.I.P Sam.

 

About this writer:


Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.