Haya ndiyo maneno Halima Mdee alimjibu Askofu Gwajima baada yake kumkashifu mitandaoni

Mbali na kuhubiri, Askofu Gwajima amekuwa akizungumzia mambo mengi yanayohusu Tanzania. Alianza na Diamond na leo aliongelea mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye alihutumiwa kwa kutoa lugha chafu bungeni.

Hivi ndivo alivyomweleza:

“Kwenye bunge kulitokea mbadilishano wa maneno kwenye uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki, inaonekana kuna mahali Chadema hawakutendewa vizuri. Kwenye mabishano hayo mbunge wangu wa Kawe akamwambia spika ‘wewe ni fala.’ Halima hilo jambo si sawa, hilo jambo sio sawa hatuwezi kukemea wengine wewe tukakuacha hilo jambo sio sawa. Ni kweli uliudhika, ni kweli ulikasirika lakini namna ya kuonyesha hasira yako sio kumtukana mtu ambaye ni mtu wa muhimili, ili Tanzania iwe vizuri nenda kaombe msamaha yaishe,”alisema.

“Ni lazima mtu yeyote anayeongoza wananchi awe mfano kwa maneno, vitendo na kwakuwa na moyo wa kuzuia hasira yake. Uwe na uwezo wa kubeba mambo, ukishindwa kujizuia na kumtukana Spika, watoto wanaosikia wanadharau nchi.”

Aidha alisema mbunge huyo kuwa hata kama aliudhika ni afadhali angejiangusha chini na kupiga kelele kuonesha hasira yake na si kutukana. Aliendelea kwa kuongeza kuwa “Koma, acha, wewe ni mbunge mzuri na mimi ni rafiki yako nakuambia ukome kumuambia maneno mabaya Spika.”

Na Halima Mdee akamjibu hivi:

“Namuheshimu sana Mch.Gwajima,sitajibizana nae kwenye mitandao. Niweke rekodi sawa sijamtukana na wala sitarajii kumkosea heshima Spika. Hayo ya J2 namwachia yeye! Yangu na yaliyojiri Bungeni.. Najua jinsi ya kuyahandle. Yawezekana yalishamalizwa kabla ya Ibada yake LEO.”

“Usinigeuze maji kesho, mana nakujua mzee wa single touch ukimuamulia mtu” Diamond amkejeli Askofu Gwajima

Beef kati ya Diamond na Askofu Gwajima ilianza baada ya askofu huyo kudai kuwa Diamond ni mshirika wa dini la kishetani la Freemasonry.

Askofu huyo alisema kuwa Diamond anamuimba kwa nia mbaya, aliapa kuwa angegeuza staa huyo kuwa maji lakini alibadilisha nia yake baada ya Diamond kumwomba msamaha.

“Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba?….. lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: “mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea….ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea…

“Point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma, lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa chini na kumaliza…nawote kufurahi kwa pamoja, lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikua anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana…ikapelekea hadi kufikia hapa…asa hapo kosa langu mie liko wapi??

“Chonde chonde mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho ?, mana nakujua mzee wa single touch ukimuamulia mtu……. naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka mzima???” Diamond aliandika kwa Instagram.

Askofu huyo alimwonya Diamond tena alipokuwa akihubiria maumini wake Jumapili iliyopita, alisema kuwa Diamond akirudia kosa lake hatamsamea tena. Tazama video hio hapo chini: