Post ya Billnass Iliyowaacha Mashabiki Katika Hamasa ya Kujua Zaidi.

Siku ya leo mida ya asubui msanii wa muziki bongo aliweka post moja ya kustua sana katika ukurasa wake wa instagram huku akiwaacha mashabiki na watu wanaomfuata kutaka kujua undani wa post hiyo ambayo haijafafanua nini hasa alikuwa akimaanisha msanii huyo.

Billnass ambae aliweka picha ya tumbo la mwanamke akiwa mjamzito na kuandika caption iliyokuwa ikumuelezea mwanamke amewashyangaza na kuwatia hamsa watu wengi huku wengi wakitaika kujua swala hilo ni kiki, mziki au mwanamke wake anategemea kupata mtoto hivi karibuni.

Billnass aliandika “umenibebea mtoto ingawa sikubebi vyema,..haina maana sikupnedi tena , natamani ulimwengu ujue ninavyokupenda na mwisho wetu hauna mipaka labda NIKUZIKE TU.’

Wengi wa mashabiki zake wanaamini kuwa bilnass anajaribu kuonyesha hisia zake kuwa mwanamke aliyenae ni mjamzito lakini bado swali linakuja kuwa  je mwanamke huyo anaweza kuwa nani, kwa sababu hapa karibuni msanii huyo alikuwa akionekana yupo karibu sana na Lulu Diva ilhali hapo mwanzo alikuwa na mahusiano na Nandy.

Billnass Atoa Sababu ya Kumpenda Sana Mama Yake.

Msanii wa bongo fleva Bilnass amefunguka na kutoa sababu ya kuwa siku zote amekuwa akimtaja sana mama yake kuliko baba yake na kwamba hata katika moja ya wimbo wake alionekana kumpondea  baba yake.

Billnas anasema kuwa amekuwa akifanya hivyo ili kuwapa moyo na motisha wamama wote na kujiona kuwa wao ni bora zaidi ili kufanya kazi vizuri kwa bidii.

Namsifia sana mama yangu ili kuwapa motisha wanawake wengine  na kuendelea kupambana  zaidi, sio kwamba baba yangu sio bora zaidi hapana lakini baba yangu ni mtu mzuri na amekuwa akinisaidia sana  na ni mtu mzuri na anaendelea kunisaidia tu  na yupo kwa ajili yangu kila siku na huwa siona kama kuna haja ya kumtaja baba kwa sababu inajulikana kuwa baba ni kichwa cha familia.

Bilnass :-‘Kutongoza Mwanamke , Its Too Old’

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Bilnass amefungua na kuweka wazi njia rahisi anayoitumia ili kuwapata wanawake anaoingia nao katika mahusiano siku zote huku akikataa swala la kutongoza ambalo kwake anaona kuwa ni kama njia ya kizamani.

Akiongea katika kipindi cha kikaangoni, Bilnass anasema kuwa mara nyingi amekuwa mtu wa kuanzisha mahusiano ya kirafiki na mwanamke anayetaka kuwa nae katika mahusiano huku  hivyo kwa sababu nakuwa tayari alishatengeneza urafiki inakuwa sio kazi kubwa kuanzisha nae mapenzi.

Mahusiano yangu mengi hayaanziagi kwenye kufukuzana,thats too old, imakaa kizamani sana naanza kwa kuwa na urafiki na huyo mtu na unajua ukishakuwa na urafiki na mtu inakuwa rahisi sana ila ile kuanza kumfukuzia mtu sijawahi.

Bilnass amekiri kuwa katika mahusiano kwa sasa ingawa hajataka kuweka wazi aliyenae sasa hivi huku akikiri kuwa alishawahi kuwa katika mahusiano na msanii mwenzake Nandy.

 

Nidhamu Inapimwaje?- Billnass Amhoji Petit

Ikiwa bado wanaendelea kurushiana maneno na kila mmoja akijaribu kujitetea ili asionekane kuwa yeye ndie mkosaji, msanii wa bongo fleva billnasi naaliyekuwa meneja wake kwa muda mrefu Petit Man wameingia katika mgogoro usiotaka kuisha kwa madai kuwa kuna mmoja alikuwa akimnyonya mwingine kimaslahi.

Huku Petit Man akilalamika kuwa Bilnass alikuwa hana nidhamu kabisa na ilifika muda alikuwa hataki hata kumsikiliza yey kama meneja wake na kujikuta akifanya mambo mengi peke yake bila kuwashilikisha wao kama uongozi, kitu ambacho kwa upate wa meneja huyo anadai kuwa swala hilo ni utovu wa nidhamu.

akijibu tuhuma hizo, msanii huyo alianza kwa kuhoji kuwa je kama mtu akitaka kupima nidhamu ya mtu anaipima kwa kutumia nini.

nidhamu inapimwaje?nimepita  kwingi sana  ambako sijawahi kuwa  na ripoti mba ya nidhamu, nilikuwa shule , nikaenda chuo miaka mitano miwili ya diploma na mitatu ya digrii lakini sikuwahi kupewa hata suspension huko kote wala kupewa ripoti mbaya ya hicho anachokisema yeye.

Nimefanya kazi na watu tofauti tofauti na wala hawajawahi kusema kuhusu nidhamu yangu kama Mr. T.

Akijibu tetesi za kuwa alikuwa anachukua hela kwa watu bila kufuata uongozi na mkataba unavyosema, billnass anasema kuwa kwa anavyojua yeye meneja ndio huwa wanatabia ya kudhulumu wasaii na sio wasanii kufanya hivyo kwa meneja.

mara nyingi meneja ndio huwa anadhukumu msanii,sijawahi kuchukua ela ila nilikuwa najitahisi sanaku-insist ela inayopatikana tufanye mtaji, kama nilikuwa nachukua ela ningekuwa tajiri sana kwa sababu kwa miaka miwili tumekuwa tukiingiza ela nyingi sana na zimetumika sana.

Alipokuwa akitambulisha wimbo wake mpya wiki iliyopita katika stesheni za radio za Clouds ,Billnass alisikika akisema kuwa imekuwa ni nafuu kwake kumuonameneja wake huyo akiondoka katika lebo yake kwa sababu amemsababishia damage kubwa sana katika muziki wake.

 

Billnass Ampa Uchebe Dhana za Kupambana na Nuh Mziwanda

Msanii Billnas amemzawadia uchebe zawadi ya vifaa vya kufanyia mazoezi huku akimwambia kuwa amefanya makusudi kumleta vifaa hivyo ili aweze kufanya mazoezi na kuwa fit ili aweze kupambana na watu wanaomfatilia mkewe Shiloleh hasa msanii mwenzao Nuh Mziwanda.

Jumamosi wikiendi iliyopita Uchebe na Shiloleh walifanya weddingparty baada ya kufunga ndoa mwezi mmoja uliopita,party hiyo ilifanyika masaki jijini Dar es Salaam ilikuwa ya kufana sana na walikuwepo  wasanii wengi wakiwemo wasanii wa kundi kubwa nchini la Wasafi likiongozwa na meneja wao Diamond platinumz.

Wakati wa kuto zawadi kila mmoja alikuwa na chake mkononi lakini kwa upande wa bilnass aliona isiwe shida bali kumsaidia uchebe kuwa fit kwa kumpa  ahadi ya kumtafutia vifaa vya mazoezi huku akimwambia afanye mazoezi ili apambane na Nuh mziwanda.

najua mwanangu ashrafu anapenda nini,anapenda michezo ya ngumi kwaio na mimi kwa kulitambua hilo  na mimi nitamzawadia vifaa vya mazoezi kwa ajili ya fitness.ufanye mazoezi hata ya kupambana na kina nuh mziwanda , sisi watoto wa kiume inabidi kujilinda pale inapobidi.-Alisema Bilnass.

Ukiachna na vikwazo vingi walivyopitia shiloleh na uchebe mpaka kufikia hatua ya kukamilisha ndoa hiyo ikiwani pamoja na kukataliwana baaadhi ya ndugu na kusema sana katika mitandao, Nuh Mziwanda alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wakiliandama sana penzi la wawili hao mpka kufikia hatu ya kutaka kuwagombanisha kwa kuvujisha picha za uchonganishi.

Nuh mziwanda alikuwa mwanaume wake na shiloleh kabla ya kukutana na uchebe, nuh alikuwa ni moja ya kikwazo sana kipindi cha maandalizi ya harusi ya wawili hao kupelekea hadi kufunga ndoa kimyakimya.

Siku hiyo ilikuwa ni moja ya siku ya bahati kwa msanii shiloleh na mme wake uchebe kutokana na zawadi nyinge walizpokea kutoka kwa wasanii wenzao  ikiwemo gari,ahadi za kusaidia katika kazi na ada za shuke kwa watoto wake.Wasanii wengi waliohudhuria waliwatakia maisha mazuri na yenye baraka katika katika ndoa yao .TUNASEMA HONGERA KWAO.

 

 

 

Billnasi Atupilia Mbali Ombi la Ndoa Kwa Nandy

Msanii wa muziki Bilnass amejibu kwa kukataa ombi la msanii mwenzie Nandy la kutaka kuolewa nae hata kama  anahisia nae .Bilnas anasema kuwa anaheshimu sana hisia za nandy lakini hawezi kufunganae ndoa kama yeye anavyotaka.Wiki moja iliyopita Nandy alisema kuwa natamani sana kufunga ndoa na msani mwenzie Bilnass kwa sabau ameona kuwa huyo ndie anasifa za kuwa mwanaume atakae ishi nae maishani.

Bilinasa anasema kuwa hawezi kujibu maombi ya Nandy  in a positive way kwa sababu anaweza kuharibu mahusiano yake kwa sasa , hivyo angeweza kujibu kama hana mahusiano lakini anamshukuru Nandy na anaheshimu sana hisia zake.

kwa comment yangu kwa sababu mtu ameelezea hisia zake, kutokana labda na perssonality yangu ila kwakweli nandy hanijui kiundani sana,siwezi kujibu in a positive way ingawa naheshimu sana hisia zake na ninaheshimu sana mawazo yake na alichokizungumza.lakini kwa sababu niko kwenye mahusiano siwezi kufanya move yoyote kwa sababu sitaki pia kujiharibia mimi mwenyewe na nina heshimu mahusiano yangu siwezi ku-comment chochote kwa sababu naogopa kumkwaza mwenzangu na hakitakuwa na mrejesho mzuri hata kidogo kwa mahusiano yangu lakini ninaheshimu hisia zangu,

Hata hivyo wawili hao wanaonekana kuvutiwa na kila mmoja kwa sababu bilnasaa alishawahi kusema kuwa nandy ni msanii wa kike ambae angeweza kuwaza awe mkewe endapo atataka kutafuta mwanamke msanii wa kuona, ndicho alichokisema Nandy hivi karibuni kuwa  Bilnas ni mwanamuziki anaeweza kuolewa nae ingawa hawezi kumfata na kumwambia.

Wawili hao walishawahi kuwa na teyesi za kuwa na mahusiano ingawa kila mmoja amkuwa akikataa kuthibitisha hilo.Wote  ni wasanii wazuri na chipukizi, inawezekana kuwa pamoja kuna weza kuwafanya kuwaongezea mashabiki na kupendwa zaidi.