Bob Juniour Awatolea Povu Wasiotaka Kuonga.

Msanii na muandaaji wa muziki nchini Bob Junior  amefunguka na kusema kuwa yeye ni moja kati ya wanaumehodari wa kuonga pesa wanawake na huku akijitamba kuwa kufanya hivyo sio ujinga bali ni moja ya sifa ya mwanaume kwa mwanamke wake.

Maneno ya Bob Juniour yameonekana katika ukurasa wake wa instagram, alipoweka video clip inayomuonyesha mwanamke akicheza moja ya nyimbo zake huku yeye mwenyewe akiwa anamwagia pesa mwanamke huyo kwa kuyarudi vizuri mauno.

katika video iyo Bob Juniour aliweka caption ” sioni shida kumuonga mwanamke pesa, mwanamke ninae mpenda kumpa pesa, gari au nyumba sio ufala ni mapenzi ya kweli, kama ujui kuonga utaibiwa sana, hongo na mhudumie mke wako ..sio unategemea ndizi tu utakuja kuibiwa shauri zenu ..endeleeni kuwa viben ten mjini mtaibiwa.

Diamond na Bob Junior Watangaza Kuja Na Kazi Mpya

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB, Diamond Platnumz na msanii mwenzake na producer kutoka Sharobaro Records Bob Junior wametangaza kuja na project mpya.

Diamond na Bob Junior ambao kwa muda mrefu wamekuwa na tofauti wameonekana kuzimaliza tofauti hizo na kuamua kufanya kazi pamoja kama zamani.

Siku ya jana kuna kuna video clip ilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Diamond na Bob Junior wakiwa pamoja na kuwataka mashabiki kukaa mkao wa Kula kwani kuna kazi wanafanya pamoja

Wasanii hao wawili walikuwa na tofauti kipindi cha katikati kwani maelewano yao hayakuwa mazuri kutokana na kutofautiana kikazi, lakini hivi sasa wasanii hao wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri.

Tunda Kanizidi Umri tu Sio Kazi:-Bob Junior

Msanii wa bongo fleva wa muda mrefu  Bob Junior amefunguka na kumjibu tunda man kuwa aache kumdharau kwa sababu kati yake na yeye  wanazidiana kwa umri tu na sio kazi kama ambavyo yeye amekuwa akimuita mdogo.

Bob Junior ameyasema hayo alipokuwa akiongea katika kipindi cha EATV,  cha eNews  na kusema kuwa yeye ameanza musiki kwa muda mrefu sana ila wazazi wake walikuwa wakimkata kufanya muziki na kuwa ekuwa akmheshimu sana tunda man kwa sababu ni mkubwa kwake kiumri na wala sio kazi.

Tunda ni kaka yangu na ninamheshimu sana kwa sababu amenizidi umru sana tu, lakini katika kazi naomba tuheshimiana sana mimi so mtoto kama yeye anavyosema kuwa mimi ni mtoto ,mbona nimemfanyia baadhi ya nyimbo zake wakati anaanza na sijasema kitu  sasa nani mdogo hapo kati yake na yangu.

Tundaman- Bob Junior Ni Mtoto Mdogo Sana Kwangu

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Tundaman ameibuka na kumtolea povu zito msanii mwenzake Lakini pia producer wa muziki Bob Junior na kudai ni mtoto mdogo sana.

Tunda man ni moja kati ya wasanii ambaye ameshawahi kufanya vizuri sana siku za nyuma na kazi zake lakini kwa muda mrefu amekuwa kimya na hajasikika akitoa ngoma na Ametaja Sababu kuwa ni ndoa yake na mtoto wake.

Baada ya kimya kingi Tunda amerudi kwa kasi ya ajabu kwani wiki iliyopita aliachia ngoma zake tatu mfululizo pamoja na video zake kwenye kipindi cha Friday Night Live.

Lakini baada ya tukio hilo Bob Junior ameibuka na kudai kitendo cha Tundaman kutoa video tatu kwa mkupuo mmoja ni kukurupuka bila kuangalia hali ikoje.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Tunda man amemjia juu Bob junior na kumuita bwana mdogo sana kwake kwaiyo hawezi kumwambia kitu:

Mimi na Bob Junior ni vitu viwili tofauti Kwanza mimi nimeanza kufanya Muziki muda mrefu Bob Junior kaja juzi juzi tu hapa 2009 sijui 2010 kwaiyo Kwenye muziki hawezi kunishauri kitu chochote kikaendana na mziki wangu ni bwana mdogo sana kwangu”.

 

 

Bob Junior Anasakwa na Polisi Baada ya Kumtembezea Kipigo Cha Mwizi Mpenzi Wake Sabrina

Mwanmuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva, Bob Junior amekumbwa na skendo mpya ya kumpa kipigo cha haja aliyekuwa mpenzi wake Muigizaji wa Bongo movie Sabrina au maarufu kama Sabby angel.

Sabrina na Bob Junior wamekuwa Kwenye Mahusiano kwa miaka zaidi ya nane ambapo inadaiwa Bob Junior amekuwa naye Kwenye Mahusiano hata kabla ya kuoa na inadaiwa hata baada ya Kumuoa aliyekuwa mke wake Halima aliendelea kuchepuka na Sabby.

Kwenye Interview aliyofanya na Shilawadu ya Clouds Tv, Sabby amefunguka na kudai Bob junior amempiga kipigo cha mwizi baada ya kumwambia anataka kuvunja Mahusiano yao kwani alikuwa haoni kama wana future pamoja.

Baada ya habari hizi kuenea Shilawadu walimtafuta na kumuuliza kama ni kweli alipoweka na Bob Junior Sabrina alifunguka:

Kweli kuna matatizo yametokea, unajua mtu huwezi kulazimisha mapenzi nikikwambia it’s over its over lakini yeye anaforce mapenzi ananipiga mambo ya zamani kwanza siku hizi mwanamke hapigwi unanipiga umenitolea mahari? Nimeona hana future nikaamua kumuacha lakini mtu hataki kuelewa anakuja ananipiga mi naona kama naonewa”.

Sabrina ameelezea kuwa Bob Junior Alifika nyumbani kwa ndugu yake na kuanza kumlazimisha kuondoka naye baada ya yeye kukataa Akaanza kumpiga Ngumi, Mateke akamkalia na kumuumiza vibaya mno.

Sabrina aliweka wazi kuwa aliamua kumuacha Bob Junior kwani ni mtu ambaye hafikirii maendeleo yeye anapenda kufanya starehe na kunywa pombe wakati yeye anataka maendeleo.

Sabrina ameweka wazi kuwa Bob Junior anasakwa na polisi kwa hivi sasahivi maana ana RB yake.

Bob Junior Aongelea Bifu Lake Na Q-Chillah,Blue Nae Atajwa

Bob junior amekuwa ni moja ya wasanii wanaoingia katika ugomvi mara nyingi tena hasa na wasanii ambao walianza chini ya lebel yake, miezi kadhaa iliyopita msanii huyu ambae pia na lebel yake, alisikika katika vyombo vya habari akizungumzia bifu lake na msanii Diamond Platinumz na kusemakuwa Diamond amekuwa akimkaushia kuwasiliana nae.

Akionge na eNews ta EATV, msanii Bob Junior ambae anafanya vizuri na kibao chake kipya kwa sasa  anasema kuwa watu wameanza kumzushia katika mitandao kuwa ana bifu zito na Q-Chillah lakini maneno hayo hayana ukweli wowote na aliamua kumuonyesha mwandishi mpaka meseji ambazo Q-Chillah amekuwa akimtumia kwa kumpongeza kuhusu kazi nzuri aliyoitoa hivi karibuni na kumpa ushauri , Bob Junior anasema”Q-Chifu ni kaka angu amenielekeza vitu vingi sana katika muziki, sina bifu na Q-Chifu,nina kazi zake nyingi binafsi, mi siwezi kugombana na Q-Chifu,kwa sababu nampenda ,ni kaka yetu wa muziki na ni baba yetu pia

Pia anasema kuwa watu wanozungumza katika mitandao kuwa Q-Chillah ameacha album shalobaro record kwa sababu ya bifu lao sio kweli na kwamba wamuache q-Chillah mwenyewe azungumze lakini sio wao.

Hata hivyo akizungumzia tetesi za kuwa yeye na .Mr.Blue wanakuwa na ugomvi kutokana na yeye kuwa anaimba kwa ku-rap kama Mr.Blue ,Bob Junior amefunguka na kusema kuwa yeye haimbi kwa kumuiga mtu yeyote , ila amekuwa akifanya kazi zake kama yeye na kwa sasa anataka kuwa na albumu mbili yaani album ya kuimba na ya kuchana lakini sio kwamba kuna mtu anamuiga.

mimi sichani kama mtu yeyote, mimi nachana kama mimi Bob Junior, mimi ninaimba sanaa,na kwanza ninampango wa kuwa na album mbili ya kuimba na album ya ku-rap, nataka niwafundishe marapper kuwa mimi ni rapper bora zaidi, mimi nina punchline hakunaga” aliongezea Bob Junior

Kuna kuwa na bifu zinazoanza chinichini kwa baina ya wasanii huku wakiwa hawana sababu ya msingi, wengine wakiingiza mambo yao binafsi katika kazi za musiki, hata kama wasanii wanakuwa wanaoneana wivu ,basi wivu huo uwapelekee kufanya muziki uendelee.

 

 

 

Bob Junior- Acheni Kuingilia Kati Bifu Langu na Diamond

Aliyekuwa Producer wa Diamond Platnumz ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongo Fleva Bob Junior, Amewataka mashabiki kuliacha kama lilivyo swala lake yeye name Diamond kwani hakuna anayejua mwanzo wa kazi zao.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya mpya ya ‘Give me’ ameiambia Bongo dot home ya Times FM kuwa mashabiki wanaingilia Kati kitu wasichokijua kiundani kitu ambacho sio sawa.

Katika mahojiano aliyofanya Bob Junior alisema;

“Ukweli ni kwamba hawapaswi kunizungumzia na yeye kwasababu kipindi tulikuwa tunatengenezana tulikuwa wawili, kwa hiyo huwezi kuingilia wewe kama shabiki maandazi kea kuingilia vitu ambavyo huvijui. Mimi na yeye  tulikuwa tunafahamiana wakati tupo chumbani, wakati chumba ni studio lakini baada ya hapo tukawa wakubwa, sasa wewe shabiki ambaye unazungumza unamjua yeye? Au unanijua Mimi? Au Mimi na  yeye ndo tunajuana vizuri name zaidi”.

Pia ameongeza Kuwa;

“Kwa iyo wewe unaingia Kati baada ya kumfahamu Bob Junior na huyo muhusika (Diamond), unanza kumtetea yeye au kunitukana mimi wakati sisi hutuwafahamu?”.

Bob Junior amekuwa akimshutumu Diamond kwa kutangaza Kuwa kuna kolabo ambayo wangefanya pamoja lakini hakuna utekelezaji wowote na amekuwa akimtafuta ili kuzungumza hilo lakini Diamond amekuwa akimpuuza.