Viongozi Wa Dini Wamjia Juu Diamond

Katika wimbo wake mpya ambao Diamond Platinumz ameimba  unaojulikana kwa jina la Hallelujah, baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu wameibuka na kuzungumzia swala hilo na kusema kuwa Diamond hajafanya vizuri kuimba  wimbo huo  kwa sababu huku ni kama kukiuka imani yake ya kiislamu na kumsujudia nabii Issa, lakini pia katika wimbo huo diamond alionekana kuvaa cheni zenye msalaba ikimaanisha anakubali kuwa kiongozi huyo wa dini alisulubiwa msalabani.

Kitendo cha kuvaaa msalaba kilichoonyeshwa na Diamondni ishara ya yeye kuonyesha kuwa anakubali kuwa nabii issa kasulubiwa, sasa si bora hatuambie kuwa yeye sio muislamu, kwanini uwaambie watu kuwa wewe ni muislamu alafu  unavaaa msalaba, na katika nyimbo zake  si bora angeimba nimbo nyinyine nyingine tu, anaimba Halleluyah” aliongea shekhe kipozeo

Halleluyah ni moja ya nyimbo mpya za Diamond ambazo zinafanya vizuri duniani kote, wimbo huo uliotoka mwezi uliopita amewashirikisha kundi la muziki la MorganHeritage .Ikiwa kama nyimbo mojawapo iliyomfanya   Diamond aendele kujulikana kimataifa na  anaona alipiga hatua kubwa katika muziki kutokana na kushirikiana na wanamuziki wakubwa Duniani, Diamond aliimba wimbo huo kwa dhumuni la kikidhi mahitaji ya mashabiki.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa msanii Diamond  na wasanii wengine kuongelewa na viongozi wa dini zao  kutokana na nyimbo wanazoimba, lakini kwa upande wa Diamond  haijawa wazi kuwa mambo hayo yote ambayo Diamond amefanya katika wimbo huo alimaanisha  kile ambacho viongozi wa dini watakuwa wamekimahanisha pia.

Bado diamond hajajibu chochote kuhusu tuhuma hizo alizoshtakiwa na viongozi wa dini yake, lakini nadhani inampasa kujibu ili aweze kuweka wazi kwa watu pia, sio tu katika wimbo huu tu , lakini pia baada ya wimbo wa Eneka  kutoka kuna baadhi ya mashabiki zake ambao waliongelea swala ya msanii huyo kuoneka akiwa amevaa cheni yenye msalaba inayoashiria  ishara tofauti na dini yake, lakini pia kuna badahi ya alama ambazo mashabiki wake walihoji Diamond kuzionyesha zilizokuwa na walakini,

Mapya Yaibuka, Nillan si wa Diamond, Wema Arudisha Majeshi Madale

Kadri siku zinavyozidi kusonga ndivyo mambo yanazidi kuwa mengi,kuna mengi yanayokuwa yamejificha  ambayo inawezekana kweli yakawa yanafanyika au watu katika  mitandao wanakuwa wanazusha tu, baada ya tetesi nyingi kuwakumba , Dari na diamond na kufikia hatua mpaka ya kutokuwa na mahusiano mazuri, bado tetesi hizio zinazidi kuwaandama wawili hao .Inasemekana kuwa  kuna taarifa za kuvuja kwa siri nzito kutoka kwa watu wa karibu wa Diamond bila yeye mwenyewe kujua.

Leo katika mtandao wa kijamii wa instagram muda mfupi uliopita kumekuwa na tetesi mpya kuhusu taarifa kuwa mtoto wa pili wa kiume wa Diamond Platinumz anaejulikana kama Nillan sio wa kwake na kuwa eti katika kipindi ambacho Diamond alikwenda kufuatilia maswala ya kipimo cha DNA na baada ya kuthibitisha kuwa mtoto huyo sio wa kwake ndipo alipoamua kunyamaza na icho chiko kilicholeta mtafaruku mkubwa kati ya mama na baba wa mtoto huyo.

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram, Mange Kimambi ambae amekuwa akionekana mtu mwenye ujua  siri nyingi za watu wengi, Mange alitoboa undani huo na kusema kuwa Diamond alipokwenda  Afrika ya Kusini  kushereka birthday ya Mama Tiffah alikwenda na kufanya DNA na  iliyoonyesha kuwa mtoto huyo w akiume  ambae ilikuwa ikisemekana kuwa ni wa diamond sio wa kwake kwa mujibu wa vipimo vya DNA.Hata hivyo Mange anasisitiza kuwa baadhi ya watu wa karibu wa msanii huyo wamekuwa wakijua siri iyo lakini wamekuwa wakinyamaza ili kulinda heshima ya msanii hyu ambae kwa muda mrefu amekuwa akikanusha taarifa hizo.

Kwa upande mwingine pia , kuna tetesi kuwa kwa sasa msanii Diamond Platinumz amerudiana na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu ambae walikuwa katika mahusiano kwa muda wa miaka kama minne nyuma .Tetesi hizo ambazo hazina ukweli bado zinadai kuwa Wema Sepetu amekuwa akionekana nyumbnai kwa diamond muda mwingi sasa na hata katika mfululizo wa sherehe za kusherkea sikukuu ya kuzaliwa kwa msanii diamond Wema Sepetu ndie alieandaa moja ya sherehe hizo.

 

Inawezekana Ni Kweli Diamond Na Zari Mapenzi Yameisha

Tunakuwa na furaha sana katika kumbukumbu za sikukuu zetu za kuzaliwa  tena hasa tunapopata salamu za upendo kutoka kwa watu wetu wa karibu, kwa Dunia hii ya sasa ya utandawazi imekuwa ni kawaida kumtakia kheri ya sikukuu ya kuzaliwa mtu wako wa karibu kwa kuweka picha yake katika mitandao ya kijamii kama Facebook , Twitter lakini hasa hasa ni ukurasa wa Instagram ambao watu wengi kwa sasa  wanautumia.

Tarehe 2  October mwaka huu ilikuwa ni siku muhimu kwa msanii Diamond Platinumz kwa sababu alitimizia miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwake,katika siku hiyo Diamond alifanya sherehe mfululizo siku tatu(pre-birthday party) akijumuika na baadhi ya ndugu na marafiki zake wa karibu.Lakini bado kunakuwa na utata kwa sababu tangu  kumeanza kwa shamrashamra hizo, mama mzazi wa watoto wa Diamond hajaonyesha muamko wowote wa kufanya lolote katika siku iyo ya kuzaliwa ya mpenzi wake.

Ikiwa ni kama wiki imepita tangu Zari afanye birthday party yake nchini Afrika ya Kusini , Diamond na team yake nzima ya Wasafi walisafiri na kwenda, je hii haikupaswa kutokea hata kwa Diamond ambae amefanya sherehe hii nchini Tanzania, je ni kweli Zari hakuona umuhimu wa kuudhulia sherehe hiyo , na je kama alikuwa amebanwa na kazi nyingi alishindwa kuonyesha upendo na furaha kwa mzazi mwenzie kwa kumpost katika ukurasa wake wa instagram ilhali akiendelea kupost picha zake? haya  ni baadhi ya maswali ambayo mashabiki wamekuwa wakijiuliza, au zile hasira za Diamond kuzaa na Hamisa Mobeto bado hazijaisha.

Ikumbukwe kuwa kusafiri kwa Diamond kwenda Afrika Ya Kusini ilikuwa ni moja ya vithibitisho kuwa wawili hao walishaweka mambo sawa, sasa je nini kinaendelea,hivi karibuni Zari na Diamond walikuwa katika majibizano ya mtandaoni kuhusu kosa la Diamond kuiri katika media kuhusu yeye kuzaa na video queen Hamisa Mobeto ilhali akikiri kuwa alikuwa anatoa hata matumizi kwa siri bila mzazi mwenzie huyo kujua chochote.

Hakuna aliyeamua kuweka wazi mpaka sasa kuhusu mahusiano yao, lakini kwa kuwa Diamond ni msanii na ana mashabiki pia, mashabiki wamekuwa na hamu kubwa ya kutaka kujua nini kinaendelea kati ya wazazi hao wawili ambao tayari walishaanzisha familia inayowahitaji sana.