“Nawashangaa Watu Wanaosema Dogo Janja Ni Mdogo “- Irene Uwoya

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amefunguka mazito kwa mumewe staa wa Bongo fleva Dogo Janja ambapo amedai kuwa ni moyo wake na kukiri kuwashangaa watu wanaosema yeye ni mdogo.

Ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya ilishangaza watu wengi ilipofungwa mwaka jana mpaka hivi sasa kuna watu ambao hawaamini kuwa wawili hao wameoana.

Na imekuwa ngumu kwa watu wengi kuzoea Mahusiano hayo hasa kwa sababu tofauti kubwa iliyopo baina yao kuanzia umri mpaka vitu vingine ambavyo vinaonekana baina yao.

Lakini kadri siku zinavyozidi kuenda wapendanao hao wameendelea kuuthibitishia uma wa Watanzania kuwa wanapendana na watazidi kuwa pamoja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Uwoya kamfungukia mazito mumewe Dogo Janja ambapo amekiri kuwa anampenda mumewe na kusema anawashangaa watu ambao wanekazana kumsema ni mdogo kwani yeye anamuona mtu mwenye akili sana:

Nakupenda sana sijawahi kukutana na mwanaume mwenye akili kama wewe na muelewa kama wewe….mdogo lakini mmmnh mimi ndio ninajua ndio maana wakiongea nawaangalia tu nasema iiiiii Dogo Janja wewe ndiye moyo wangu”.

Dogo Janja naye anaonekana amekolea na penzi la Irene kwani mara kwa mara anamposti mkewe na kumwagia sifa lukuki kama mke mwema na mwaminifu na kadhalika.

“Dogo Janja Sio Mwanaume Wa Dar”- JCB

Mwanamuziki mkongwe wa Hip hop toka Arusha JCB amefungukia ishu ya Dogo Janja kumuoa Uwoya na kusema siyo mwanaume wa Dar kama watu wengi wanavyofikiria.

JCB amefunguka na kumsifia Dogo Janja baada ya kufanikiwa kumuoa mtoto mzuri kama Wolper na kudai amewababr watu wa Arusha na kusisitiza kuwa Dogo Janja sio mtu wa Dar.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, JCB amefunguka na kumsifia Dogo Janja kwa kitendo chake cha kufanikiwa kumuoa Irene Uwoya:

Unajua kwa Dogo Janja kumuoa mama kama yule pale ametupa Big up na kutupandisha na kutufanya sisi watu wa kaskazini sio wanaume wa Dar yaani tuna nguvu kwa upande huo tu wa kuwa na yule mwanamke yaani Nampa Big up sana Dogo kama anamchukua yule mtoto ametuwakilisha watu wa Arusha vizuri”.

Lakini Pia JCB alipima uzito suala la Dogo Janja kujigeuza mwanamke kwa ajili ya video yake ya wimbo wake wa Wayu wayu ambapo ameweka wazi kuwa hajui Dogo Janja alikuwa anafikiria nini kufanya vile lakini kile ni kitendo ambacho hawezi kufanya.

Irene Uwoya Azidi Kukolea Kwa Dogo Janja Achora Tatoo Ya Jina Lake

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya ameonekana kuzidi kukolea kwa penzi la mume wake Msanii wa Bongo fleva Dogo Janja kwani jana ameonyesha tattoo ya Jina lake aliyochora.

Siku za hivi karibuni Uwoya na Dogo Janja wameonekana kuweka mambo yao hadharani kidogo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu tangu ndoa yao ifungwe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Dogo Janja ameanika tattoo hiyo iliyochorwa na Uwoya kwenye maeneno ya bega iliyoandikwa Jina halisi la Dogo Janja ambalo ni Abdul.

Dogo Janja amemshukuru mke wake kwa kuchora tattoo ile na kumtaka amchoree tattoo nyingine lakini safari hii iwe kwenye maeneo nyeti kabisa.

Irene Uwoya ni Mzuri Lakini Huyo Dogo Janja Simjui- Msami

Maanamuziki wa Bongo fleva na Dansa maarufu Bongo Msami Baby amezidi kutengeneza headlines Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuendelea  kupostiana na Ex wake Irene Uwoya.

Uwoya na Msami wameendelea kuwaacha watu midomo wazi baada ya kuendelea kupostiana Kwenye mitandao ya kijamii na kusifiana ilihali Ikiwa ni wazi kabisa kuwa Uwoya ni mke wa staa wa Bongo fleva Dogo Janja.

Ishu hii imeleta tafsiri tofauti kabisa hasa ukizingatia kuwa Uwoya ni mke wa mtu na hivyo kusababisha ndoa ya Uwoya na Dogo Janja kukosa heshima mbele ya Jamii.

 

Msami amefanya Interview na Enews ya EATV na kudai haoni kama ni kosa yeye kumsifia Ex wake na kumkubali kama ni mzuri kwani ni ukweli mtupu na haoni kama kamvunjia heshima:

Irene kaniposti kwa sababu anapenda ninachokifanya na ananikibali kwa nini asiseme na mimi kumuandika kama yeye mzuri kwani ni dhambi? sio dhambi kumwambia mtu yeye ni mzuri kwangu mimi binafsi naona kama ni upendo Alafu isitoshe mimi Namjua Yeye huyo mtu wake mwingine mimi simjui mimi najuana na Uwoya tu kwaiyo tuna maisha yetu na stori zetu ambazo tunaongea”.

Msami amesisitiza kuwa hawezi kuacha kuongea na Irene au kumsifia kisa tu ameolewa na haoni kama ameandika kitu kibaya.

Msami Amefungukia Bifu Lake na Irene Uwoya

Dancer na msanii maarufu Msami Baby amefunguka na kuongelea sakata linaloendelea kutengeneza headlines hivi sasa kati yake na staa wa Bongo movie Irene Uwoya.

Msami na Irene Uwoya walishawahi kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi miaka ya nyuma lakini walikuja kuachana na Uwoya amemshirikisha kufunga ndoa na staa wa Bongo fleva Dogo Janja.

Uwoya na Msami walirudi kwenye headlines za mitandao ya kijamii siku ya juzi baada ya Uwoya kuposti maneno yenye utata na kisha Msami naye kumjibu kwa kejeli kuhusu ndoa yake jambo lililozua maneno na watu kufikiri labda wana bifu.

Msami ameongelea suala hilo Kwenye Interview aliyofanya na Soudy Brown kwenye You heard ya XXL:

Mbona mimi sijaona kibaya pale alichoposti Irene mimi naona kama kanisifia kuwa The best dancer in Africa ? Mbona mimi naona kama hajanipaka yaani hajanidhihaki”.

Msami amesema hajui kuhusu ndoa yake hata kama ameolewa lakini hajawahi kumwambia kuwa ameolewa na hata wakikutana hawaongei kuhusu ndoa yake na kuhusu kumposti amesema labda Irene anamiss maudambwi dambwi yake.

 

Irene Akizaa na Dogo Janja Huyo Mtoto Hanihusu- Mama Irene

Ndoa ya Mwanamuziki wa Bongo fleva Dogo Janja na staa wa Bongo movie Irene Uwoya imezidi kuwa gumzo Kwenye mitandao ya kijamii kwani Mama yake mzazi na Uwoya amezidi kuikataa ndoa hiyo.

Siku ya jana taarifa zilienea kuwa Mama mzazi wa Irene Uwoya alisema hamtambui Dogo Janja kama mzee wake kwani hana adabu na hajafuata taratibu za kumuoa binti yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na XXL ya Clouds Fm siku ya jana Mama Uwoya amesisitiza kuwa familia haitambui ndoa ya Uwoya kwa sababu hawakushirikishwa kwenye ndoa hiyo hivyo mume wanauemjua ni marehemu Ndikumana ambaye mpaka anafariki alikuwa ndiye mume wake halali.

Lakini Mama Uwoya pia ameweka wazi kuwa hataki kuhusishwa na ndoa hiyo kwani haimuhusi kwaiyo Hata kama wakizaa mtoto yeye hamuhusu maana hamtambui Dogo Janja:

Sasa kwani mtoto akizaa anakuwa wa kwangu si wa Irene na huyo bwana ake mimi nahusika kitu gani labda”.

Mama Irene Uwoya amesema kitendo cha binti yake kubadilisha dini hakitambui na kama watataka baraka za wazazi basi wataenda kwa wazazi waliosimamia harusi yao kwani wao hawajui lolote na wala hawakupewa taarifa ya ndoa.

Dogo Janja Awatolea Povu Zito Wanaoiponda Ndoa Yake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Dogo Janja amewajia juu watu wote ambao bado wanaiponda ndoa yake na Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya.

Ndoa hii imezidi kutengeneza headlines kila kukicha pamoja na kwamba ilifungwa mwaka jana mwishoni na ndio ilikuwa stori ya kufungia mwaka lakini bado mpaka leo hii Ndoa hiyo imebaki kuwa gumzo.

Dogo Janja amedai kuwa amechoshwa na watu wote wanaomsema vibaya kuhusu ndoa yake na Kwenye mahojiano na Enews Dogo Janja amesema nyimbo yake ya Wayu Wayu ni ujumbe kwa wale watu wote wanaomsema vibaya kwa kufunga ndoa na Uwoya.

Walitokea watu walikuwa na kejeli na nini mimi naonekana kidagaa sina chapaa wananitukana nini lakini mwisho wa siku nawakanyaga kama soksi zangu ilikuwa kama sehemu ya kufikisha maudhui kwa watu waendelee kuheshimu mahusiano ya mtu wasiangalie utofauti wowote kwenye mahusiano kinachotakiwa sana ni upendo kama watu mnapendana mnaheshimiana hivi vitu vingine ni vitu vya kawaida”.

Lakini pia Kwenye mahojiano hayo Dogo Janja alimtolea povu zito Rapa Young Tusso aliyemwambia ameidhalilisha Arusha kwa kuvaa kama mwanamke kwenye video yake ya Wayu Wayu, Dogo Janja amesema hamfahamu Young Tusso na itakuwa vizuri kama ataendelea kuwa shabiki wake.

Uwoya: Tangu Niolewe na Dogo Janja, Wanaume Wameongeza Kasi Ya Kunitongoza

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara, Irene Uwoya amefunguka na kudai tangu Afunguka ndoa na staa wa Bongo fleva, Dogo Janja amekuwa akisumbuliwa sana na wanaume wanaomtaka kimapenzi.

Irene Uwoya na Dogo Janja walifunga ndoa ya kushtukizia mwishoni mwa mwaka jana mwishoni, ndoa iliyofanyika kwa siri kubwa baada ya kukataa kuwa kwenye mahusiano kwa mwaka mzima.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Leo Tena ya Clouds FM, Irene Uwoya amefunguka na kusema anashangazwa na idadi kubwa ya wanaume ambao wamekuwa wakimsumbua kumtongoza kwani kabla hajaolewa hakuwa akipata usumbufu mkubwa kiasi hicho.

Uwoya amedai anashangazwa na kwanini watu wanadhani kuwa yeye kuolewa na Dogo Janja kumewafanya wanaume hao kudhani kuwa ndio anatamaa na anapatikana kirahisi kiasi hicho ili hali yeye ni mke wa mtu sasa hivi.

Lakini pia ndoa hiyo imezidi kupata misuko suko kwani familia ya Uwoya imesisitiza kuwa haiitambui ndoa yao na hata kama yake amedai hamtambui Dogo Janja kama mkwewe kwa sababu hana adabu amemuoa binti yao bila taarifa.

Irene Atoa Sababu ya Mama Yake Kutohudhuria Harusi Yake.

Kama ambavyo watu wengi hawakutaka kuamini kuhusu kufunga ndoa kwa Irene Uwoya na Dogo Janja , pia yalizuka maneno kuwa mama wa urene uwoya hakuhudhuria katika harusi hiyo kwa  sababu hakupenda mwanae kufunga ndoa na Dogo Janja kwa kuwa yeye hakuwahi kuwatenganisha mwanae na Ndikumana ambae alifunga ndoa ya Irene Uwoya kanisani.

Hata hivyo Irene Uwoya amezima maneno hayo baada ya kufunguka sababu iliyomfanya mama yake kutohudhuria katika harusi yao na kusema kuwa mama yake amekuwa ni mtu wa kusafiri kila siku hivyo hakuwepo jijini ndio maana hakuweza kutokea katika harusi yao.

Hakuwepo kwaio hakuweza kushiriki kwa sababu mama yangu ni mtu wa kusafiri safiri kila siku,kwaio hakuwepo tanzania lakini ndoa yangu aliibariki kabisa.mama anenda anarudi na kazi zinakuwa nyingi kwaio hatujapa nafasi ya kutulia na kusema kuwa twende lakini ni mara nyingi mimi na yeye tunaendaga nyumba na baba anauwepo hata kama mama hayupo.-Aliongea Irene Uwoya walipokuwa na mahojiano katika kipindi cha leo tena cha Clouds Radio

Lakini pia Irene alisema kuwa marehemu mzazi mwenzie alikuwa akisema maneno mengi sana katika mitandao ya kijamii kuhusu yeye na kumnyima mtoto lakini ukweli ni kwamba alikuwa akimuona mtoto na hata mara nyingin alikuwa akitumia gari yake anapokuwa Tanzania.

 

 

Uwoya Amchimba Dogo Janja Mkwara Mzito Aliposikia Anataka Kuoa Mke wa Pili

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amemchimba bonge la mkwara mume wake staa wa Bongo fleva Dogo Janja baada ya kusema ana mpango wa kuoa mke wa pili.

Kwenye Interview aliyofanya siku ya jana Dogo Janja alifunguka kuwa kama kijana wa kiislamu ana mpango wa kuongeza mke wa pili baada ya miaka kadhaa lakini pia hakuishia hapo alisema ndoto yake ni kuoa wake wanne na anaona mpaka akifikisha miaka 50 atakuwa na wake wanne.

Habari hiyo ilitrend sana siku ya leo huku kila mmoja akiongea lake kuhusu kauli hiyo baada ya habari hiyo kumfikia Uwoya amemchimba mume wake Bonge la mkwara.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Uwoya amemjibu hivi Dogo Janja:

Ndio utajua mimi kabila gani…..Thubutu uwone Tena wasikudanganye kabisa”.

 

 

Dogo Janja- Uwoya Ana Mimba Yangu Atajifungua Muda Wowote

Mwanamuziki wa Bongo fleva Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa mke wake Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya ni mjamzito hivi sasa na wakati wowote anaweza akajifungua mtoto wao wa kwanza.

Dogo Janja hivi sasa anatamba na wimbo wake mpya uonaoitwa ‘Wayu wayu’ uliojizoelea umaarufu baada ya yeye mwenyewe kuwa video queen humo ndani akiwa amevaa kama mwanamke na kupaka make up kitendo kilicho amsha hisia za watu wengi.

Kwenye media tour anayoendelea kufanya hivi sasa Dogo Janja alitua Times Fm ambapo kwenye mahojiano aliyofanya na Lil’Ommy katika kipindi cha The playlist alifunguka kuhusu mkewe kuwa mjamzito:

Inshallah si mbali toka sasa tutapata mtoto wetu wa kwanza kwa sasa mke wangu ni mjamzito hivyo tunazidi kumuomba Mungu mtoto wetu afike Salama kwa mapenzi yake”.

Lakini pia Dogo Janja aliweka wazi kuwa endapo atazaa mtoto wa kiume basi atapendelea kumuita Aboubakary jina la marehemu baba yake lakini endapo atakuwa wa kike basi atamuachia mama yake ampe jina.

“Tuolewe na Wazee Watufie?” Riyama na Uwoya Kuhusu Kuolewa na Viben- 10

Muigizaji wa Bongo movie Riyama Ally amefunguka kuhusu kuolewa na mwanaume ambaye ni mdogo kwake kiumri ambapo amesema haoni tatizo na pia kuhusu Irene Uwoya kuolewa na Dogo Janja amesema ndio vizuri waolewe na wazee wawafie?.

Riyama Ally ameolewa na Mwanamuziki wa Bongo fleva anayejulikana kama Leo Mysterio ambaye kiukweli kabisa ni kiben10 kwake kwani ana umri mdogo kuliko yeye jambo ambalo Riyama amesema ndio anapenda hapendi wazee.

Riyama na Mume wake

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Millard Ayo Tv, Riyama amefunguka na kusema kwamba haoni tatizo kuwa na mwanaume mdogo na hata alipoulizwa kuhusu rafiki yake Irene Uwoya kuolewa na kiben-10 Dogo Janja amedai ndio vizuri kutafuta kijana.

Irene Uwoya na Mume wake Dogo Janja

Kwenye mahojiano hayo Riyama alisema mambo haya:

Mimi nimempa ushauri Irene kama dada yake na rafiki yake nikamwambia kaza hapo hapo kwenye ndoa yako usilegeze maneno yatasemwa sana kama mimi ninavyosemwa kuolewa na Mume wangu niliyemzidi umri kwa sababu mapenzi furaha bwana kama furaha yako ipo hapo basi inatosha kwanini tukatafute wazee waje watufie ndani?”.

 

“Dogo Janja Kaolewa na Uwoya”- Edu Boy

Msanii wa Bongo fleva anayekuja kwa kasi kwa staili yake ya kurap Edu Boy amevunja ukimya kuhusiana na bifu linaloendelea kati yake na staa wa Bongo fleva Dogo Janja.

Siku za hivi karibuni wawili hao waliingia kwenye bifu kali baada ya kuanza kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii na kisha baadae kufanya Interview na kurushiana vijembe.

Sakata hili lilianza mara baada ya Edu Boy kutoa wimbo wake mpya ulioenda kwa jina la ‘Tunasafisha’ ambapo ndani ya wimbo huo aliwachana wasanii kadhaa huku Dogo Janja akiwa mmoja wapo.

Kwenye Interview aliyofanya baadae Dogo Janja alisema kuwa hawezi kujibu anachokiimba wala anachokisema Edu Boy kwa sababu ni mtoto mdogo sana kwake hivyo astahili jibu lake.

Edu Boy ametoa povu kali alipokuwa anahojiwa na East Africa Tv ambapo amedai kuwa Dogo Janja ameolewa na mtu mzima ndio maana anajiona na yeye mkubwa:

Dogo Janja nimepata taarifa yake nilimuona na nikasikiliza pumba zake alizokuwa anaongea mwisho wa siku nikaona yule ni Dogo tu siwezi nikamuita mdogo maana amefikisha miaka 18 ni mdogo wangu tu lakini naona kuolewa ndio kunampa mapembe na kuna vitu vingine anakuwa anachukulia poa ni ndoa ndio inamsumbua”.

Lakini pia kwenye wimbo huo huo alimchana msanii rapa Stamina ambapo baada ya kusikia amedisiwa Stamina alimtumia ujumbe kuwa akikutana naye sehemu yoyote lazima amtembezee kichapo jambo ambalo Edu Boy amedai haogopi kwani Stamina hawezi kumfanya chochote.

 

Dogo Janja na Irene Uwoya Ndani ya Mahaba Mazito

Mwanamuziki maarufu wa Bongo fleva Dogo Janja ameonekana akiweka wazi hisia zake na penzi lake kwa mke wake wa halali kabisa muigizaji wa Bongo movie mrembo Irene Uwoya.

Dogo Janja na Irene Uwoya walifunga ndoa ya siri siri mwaka jana mwishoni baada ya kuwa na mahusiano ya siri kwa kipindi cha muda mrefu, ambapo kwa kipindi chote hicho kila mmoja kwa wakati wake alikuwa anakataa kuwa na mahusiano na mwenzake.

Wawili hawa walizua gumzo na waliufunga mwaka 2017 baada ya kubainika kuwa wamefunga ndoa ya siri ambayo ilihudhuriwa na watu wachache kupita kiasi. Habari za ndoa ya mastaa hawa wawili iliwashtua watu wengi kwani waliamini kwamba wawili hawa hawaendani kwa kwa kila kitu.

Dogo Janja na Irene Uwoya wakioneshana mahaba

 

Lakini hata baada ya kufunga ndoa hawajawa watu wa kuonyesha mapenzi yao hadharani kwani wameonekana hadharani mara moja tu ambapo walienda pamoja kwenye harusi ya Shilole na Uchebe. Pia hata kuposti picha wakiwa wmepiga pamoja hawajawahi kuposti jambo ambalo wenyewe wamesema hawataki ndoa za mitandao.

Pamoja na hayo wapendanao hawa wawili wakiwa maisha yao ya kimapenzi chini ya kapeti maisha yao ya kisanaa wameamua kuyaweka yote hadharani ambapo hivi karibuni Dogo Janja ameweka wazi kuwa kuna nyimbo yake mpya inatoka hivi karibuni ambayo anemshirikisha mkewe Uwoya ambapo amedai kuwa Irene anaimba na kurap ndani.

Mama Uwoya Akana Kumjua Dogo Janja, Asema Mwanae ni Mjane.

Mama mzazi wa msanii Irene Uwoya amekataa kumjua inayesemakana kuwa ni mume wa mwanae wa kike Irene Uwoya ambae  alifunga ndoa mwishoni mwa mwaka uliopita na msanii mwenzie Dogo Janja .Mama huyo amesema kuwa anachojua yeye ni kuwa mwanae wa kike ni mjane kwa sababu mumewe wa ndoa amefariki mwaka jana na mwanae hajaolewa tena.

Irene Uwoya alipofunga ndoa ya kiislamu na msanii Dogo Janja alikuwa katika ndoa ya kanisani na mwanasoka Ndikumana na walikuwa hawajaachana lakini walikuwa katika mgogoro ambao walishindwa kuutatua mpaka mwanasoka huyo alipopatwa na umauti.

Mama Uwoya nasema kuwa anajua Irene ni mtu mzima lakini yeye atambui ndoa yake kwa sabau hakuna ndoa ambayo inafungwa bila wazazi kuhudhuria katika ndoa hiyo.anachojua ni kuwa Irene mumew amefariki.

ngoja nikwambie hakuna ndoa ambayo wazazi hawashirikishwi, ndoa yoyote lazima wazazi wajue na washiriki.ninachojua kuwa irene ni mjane, mumewe ambae sisi tunamjua ndo huyo ameshafariki.ninachojua mimi ni kuwa swala la ndoa lazima watu wazazi washirikishwe kuanzi mwanzo hadi mwisho.

Hata hivyo mama huyo anasema kuwa kama Irene ni mtu mzima basi anajua kitu anafanya hivyo hawawezi kumzui na kumkataza lakini kitu cha kujua ni kwamba wazazi hawakuwahi kuapata taarifa kuwa mtoto wao alipewa talaka na mwanaume aliyefunga nae ndoa na kwa sababu wao sio waut wa kufatilia vyombo vya habari hawakutaka kufatilia maswala ya media , walitaka kusikia kutoka kwake.

tunachojua mwanetu ni mjane,kama ana ndoa anaijua yeye lakini sisi hatuitambui na wala hatuaamini.wala hatumjui huyo mtu anaitwa Dogo Janja labda wanaigiza.

Kwa habari na tetesi zilizopo kwa sasa ni kwamba msanii huyo wa kike kwa sasa ni mjamizito.

 

 

Uwoya Adaiwa Kunasa Mimba ya Dogo Janja.

Ikiwa ni miezi kadha imepita tangu kufanyika kwa harusi ya mastaa wa bongo movies Irene Uwoya na star kutoka bongo fleva Dogo Janja , ndoa hiyo ambayo ilikuwa na walakini  na kusemekana kuwa ilikuwa ndoa ya kuigiza wakitaka kuweka kipande hicho katika tamthiliya mpya ambayo Irene anacheza inayojulikana kama Sarafu , imezaa matunda baada a wasanii hao kutegemea kupata mtoto hivi karibuni.

Akiongea na gazeti la GPL,moja ya mtoa habari na mtu wa karibu wa Irene Uwoya alisema kuwa  ndoa ya Irene na Janjaro ilikuwa sio ndoa kama watu walivyokuwa wanafikiria lakini wawili hao ni kweli walikuwa katika mahusiano  lakini hawakuta watu wajue hivyo hata mimba ambayo Uwoya anayo  wanafanya siri tu na hata Irene amekuwa akijificha nyumbani kwa rafiki yake Agnes Masogange.

ile ndoa ilikuwa ni ya kwenye tamthilia ya sarafu lakini pale bwana mdogo anapiga kweli lakini ilitakiwa iwe siri,na inavyosikia ni kuwa mdada huyo sasa hivi ni mjamzito.

Irene hakuwahi kutaka kufanya watu wajue kuwa alikuwa na mahusiano na Janjaro nandio maana muda wote alikuwa akikana kuwa hana uhusiano na Dogo lakini itakuja kujulikana tu licha ya kuwa Dogo yeye alishatangaza kumuoa Irene.

Hata baada ya kumtafta kwa muda mrefu waliamua kumuliza mtoa taarifa huyo kuhusu upatikanaji wa irene uwoya na mtoa taarifa huyo akasema kuwa mara nyigi amekuwa akishinda kwa agnes masogange .”Ebu jaribuni kwa masogange maana nasikia ndio kajificha huko” .

Waandishi wa habari waliamua kumfatilia irene kwa agnes na walipofika walikaribishwa na mfanyakazi wa ndani,walipouliza uwepo wa irene dada huyo alijibu kuwa yupo lakini laipoend ndani kumuita alirudi na kusema amelala.